Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe.Halima Omari Dendego ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Mkalama kwa kupata Hati inayoridhisha kwa Hesabu za mwaka 2022/2023 kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Pongezi hizo amezitoa Juni 28,2024 katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani uliokaa kwa ajili ya kujadili Majibu na Utekelezaji wa Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2022/2023 uliofanyika katika ukumbi wa Sheketela wilayani Mkalama.
“Nawapongeza sana kwa kupata hadi inayoridhisha, pia nawapongeza sana kwa makusanyo ya mapato.Naombeni msizalishe hoja bila sababu, atakayezalisha hoja atawajibika kujibu hoja husika pekee yake” Mhe. Dendego
Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt Fatma Mganga ameitaka kamati ya Fedha na Mipango kuweka utaraibu wa kujibu hoja kwa kila mwezi,“Katika Halmshauri zote sita mkoani Singida, nyie mmepiga bao kwa kuwa na hoja chache,hongereni sana lakini niwaombe kamati ya Fedha na Mipango muweke utaratibu wa kujibu hoja kila mwezi,” RAS Mganga
Awali akiwasilisha majibu na utekelezaji wa hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Bi. Asia Messos amesema halmashauri ilipokea taarifa yenye hoja 43 kati ya hoja hizo, hoja 29 zimefungwa na hoja 14 zilizobaki zipo katika hatua ya utekelezaji
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.