Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Mosses Machali leo Juni 3 2023 amekabidhi hati za Kimila 208 kwa wananchi wa Kitongoji cha Midibwi Kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza ambapo amewataka kutunza hati hizo kwani zina manufaa makubwa kwao.
Akiongea wakati anakabadhi hati za kimila kwa wananchi Mhe. Machali ameongeza kuwa mpango wa matumizi bora ya Ardhi ya kijiji ni suluhisho la Migogoro ya Ardhi kwa wananchi ambayo pia itazuia matumizi yasiyosahihi ya Ardhi.
‘’ hizi Hati ni dili kwanza itasaidia kupunguza migogoro ya Ardhi, pili itasaidia kupata hata mikopo Benki kwahiyo zilindeni msiziandike andike ikiwezekana tafuteni bahasha maalumu kabisa kwaajili ya kuzihifadhi’’ Alisisitiza Dc Machali.
Pamoja na hayo amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyobora kwakutenga fedha kwaajili ya upimaji wa Ardhi na kuwa na matumizi bora , hivyo kuwataka wananchi ambao hawajapimiwa maeneo yao kutumia fursa hiyo Adhimu ili kila mmoja apate hati hizo za Kimila na kuwataka wananchi kuheshimu na na kufuata mpango bora ya ardhi katika maeneo yao.
Akiongea kwa niaba ya Wananchi Diwani wa Kata ya Mwangeza Mhe. Bosco Samweli amemshukuru Mkuu wa Wilaya kufika katika kijiji cha Midibwi na kukabidhi hati hizo za Kimila ambapo ameiomba Serikali kuhakikisha wanatatua migogoro yote ya Ardhi Wilayani hapa ili wananchi waweze kupata hati za Kimila na kutumia muda mwingi kujiletea maendeleo kuliko kutatua migiogoro na kushughulikia kesi.
Baadhi ya Wananchi waliopata hati hizo wameishurukuru serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais ( Mazingira) kupitia Mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame kwakuwa na mpango wa matumizi bora ya Ardhi na kusema mpango huo utachochea kukua kwa uchumi wao binafsi na wa Kijiji kwani watatumia hati hizo kuomba mikopo na kuharakisha maendeleo yao.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.