Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Peter Masindi amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhe. James Mkwega kwa uongozi wake imara katika kusimamia miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka 10 toka kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo.
Kauli hiyo ameitoa Novemba 29/11/2023 wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama iliyofanyika katika ukumbi Sheketela uliopo katika Halmashauri hii.
“Mhe. Mwenyekiti hauko hapa kwa bahati mbaya. Leo tunaadhimisha miaka 10 ukiwa Mwenyekiti wa Halmashauri. nakupongeza sana. Leo Mkalama inakusanya Bilioni 1.7, uko imara sana”. Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Peter Masindi
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya Mkalama, Ndugu Daniel Tesha, amesema kwa kipindi cha miaka 10 toka kuanzishwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imefanikiwa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Sh. Milioni 247 kwa 2013/14 hadi bilioni 1.7 kufikia sasa.
Tesha amesema katika kipindi cha miaka 10, halmashauri hiyo imepata hati safi mfululizo miaka tisa na hati moja yenye mashaka. Wilaya Mkalama ilianzishwa Julai 2012 baada ya kumegwa kutoka Wilaya Iramba.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.