Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo amezitaka jumuiya za watumia Maji wilayani hapa kuwapa muda wahasibu wanaoajiriwa kwenye jumuiya zao ili kujiridhisha na Utendaji kazi wao huku akiwaonya kuacha kupeana kazi kwa kujuana.
Aliyasema hayo June 15 mwaka huu wakati akihutubia Katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa wadau wa Maji wilayani Mkalama.
Aliendelea kusema kuwa ili jumuiya zifanye vizuri lazima ziwe na malengo na usimamizi mzuri wa miradi ya maji huku elimu ikiendelea kutolewa kwa jamii ya namna ya kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kumnufaisha Kila Mwananchi na kutatua kabisa tatizo la upatikanaji Maji wilayani hapa.
"Ninakupongeza Meneja pamoja na jumuiya za watumia maji hakika mnafanyaje kazi nzuri sana hadi Sasa hali ya upatikanaji Maji safi na salama wilayani ni asilimia 67.17 na hapa tupo 2022 naimani ikifika Mwaka 2023 uhakika wakufikisha asilimia 85 utakuwepo na tukiendelea hivi kabla ya mwaka 2025 tutakua tumefikia asilimia 100". Aliongeza Dc Kizigo.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji Wilaya Mkalama Meneja wa RUWASA Mhandisi Antidus Muchunguzi alianza kwakuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutenga Bill 2.3 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwaajili utekelezaji a miradi ya maji wilayani Mkalama kuwa bajeti hii itachochea kuongeza upatikanaji wa huduma ya Maji na kutimiza adhima ya Serikali ya kumtua Mama ndoo kichwani.
Aliendelea kusema hadi Sasa RUWASA Wilaya ya Mkalama imehuisha na kusajili vyombo vya watumiaji Maji 20 huku akisema wanaendelea na kazi ya kuunda na kusajili jumuiya kwa miradi ya Nkungi pamoja Kinampundu inayotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni Mwaka huu.
Muchunguzi alisema kwa Mwaka 2021/2022 ofisi ya RUWASA Wilaya ya Mkalama ilipanga kuchimba visima 11 katika vijiji vya Nkalakala, Nkungi, Matongo, Nkinto, Mwangeza Lukomo, Mwanga, Ilunda, Kinankamba na Kisuluiga na tayari visima vinne vimechibwa katika vijiji vya Malaja, Nkalakala , Iambi na Mdilika huku Mkandarasi akiwa yupo site na kazi inaendelea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama James Mkwega alizitaka jumuiya kutembea kwenye malengo na kuleta mabadiliko katika jamii huku akisema haina haja kuendelea kufanya kazi kwa jumuiya ambazo hazifuati sheria na taratibu za uendeshaji .
Upatikanaji wa Maji wilayani Mkalama Kwa Sasa ni asilimia 67.17 sawa na Wananchi 161,405 wanapata huduma ya Maji kati ya wananchi oye 240,299 na huduma hii hutokana na vyanzo vya Maji chini ya Ardhi ambavyo ni visima virefu, vifupi na vya kati.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.