Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Moses Machali amewataka wazazi katika kijiji cha Mwangeza wilayani Mkalama kuhakikisha wanachangia chakula shuleni katika kuboresha mazingira ya wanafunzi kujifunza na kupelekea kuongezeka kwa ufaulu wilayani Mkalama.
Kauli hiyo ameitoa Julai 16,2024 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mwangeza kwa ajili ya kusilikiza na kutatua kero zinazowakabili wananchi wa kijiji hicho.
"Kila mzazi anapaswa kuchangia chakula shuleni watoto wasome vizuri, ambao hawatachangia wachukuliwe hatua za kinidhamu" Machali
Aidha Mhe. Machali amepiga marufuku mashamba ya shule kukodishwa kwa wananchi wengine badala yake yatumike kwa ajili ya kulima chakula cha wanafunzi.
"Marufuku kukodisha mashamba ya shule, tumieni mashamba kulima chakula cha wanafunzi ili tuweze kupunguza hata gharama za kuchangia chakula shuleni" Machali
Mbali na hilo, Mhe. Moses Machali ameagiza kuvunjwa mara moja kwa kikundi cha Nkiri kilichoanzishwa bila kuzingatia sheria na taratibu za nchi na kuliagiza Jeshi la polisi kuwakamata wale wote watakaokiuka agizo hilo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.