Meneja wa TARURA Wilaya ya Mkalama Mhandisi Mang'ara Magoti amesema kuwa Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imepanga kutumia kiasi cha Tsh. Bilioni 2,201,880,000 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za matengenezo ya Barabara Wilayani hapa .
Amesema hayo mapema Leo katika mpango wa kujadili bajeti ya utekelezaji wa shughuli za matengenezo ya Barabara ya wakala wa Barabara za vijijini na mijini Tanzania (TARURA) Wilaya ya Mkalama Kwa mwaka 2022/2023 ambao ulijadiliwa na Baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Mhandisi Magoti ameongeza kuwa matengenezo hayo yataanza Julai 2022 Hadi Juni 2023 ambayo yatahusisha mfuko wa Jimbo, tozo ya mafuta pamoja na fedha kutoka mfuko wa Barabara ( Road Fund Board) huku akieleza mchanganuo wa namna ya matengenezo hayo yatakavyofanyika kuwa ni ya Muda Maalumu kilomita 17, matengenezo ya maeneo korofi kilomita 33.135 , matengenezo ya kawaida Kilomita 33. 90 pamoja na Ujenzi wa madaraja, Drift na karavati ili kuboresha Miundo mbinu ya Barabara za Wilaya ya Mkalama ziweze kupitika Kwa kipindi kirefu cha mwaka.
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani waliunga mkono bajeti hiyo huku wakimtaka Mhandisi wa TARURA Wilaya ya Mkalama kuhakikisha wakandarasi waanza utekelezaji wa miradi hiyo na kukamilika Kwa wakati ili kuharakisha maendeleo ya Wilaya ya Mkalama na kufanya shughuli za kiuchumi kuendelea Kwa Kasi kubwa.
Aidha wameridhia Kwa pamoja na kuweka sheria Kali Kwa mtu yeyote atakayeharibu Miundo mbinu ya Barabara Kwa kupitisha Ng'ombe barabarani, kuvamia hifadhi za Barabara na kufanya shughuli za kilimo na ujenzi kuwa watachukuliwa hatua Kali kwani kwakufanya hivyo watafanya Barabara kudumu kwa Muda mrefu ambapo Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika matengenezo hayo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki Mhe. Francis Isack Mtinga ameishukuru serikali ya awamu ya sita kuona ipo haja ya kuwashirikisha Madiwani katika kujadili mpango wa bajeti ya matengenezo ya Barabara Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 hivyo kuwataka waheshimiwa Madiwani kuwa wavumilivu kwani miradi haitafika Kwa wakati Mmoja kwa maeneo yote huku akiwataka kutoa ushirikiano pindi wakandarasi wanapokuwa kwenye maeneo yao ya utawala kwa kusimamia shughuli hizo pamoja na ubora wa miradi na kuhakikisha wanasimamia Wananchi wanaoharibu Barabara kutokana na shughuli zao za kila siku.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.