Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos amewataka wananchi wa Kijiji cha Gumanga,Kata ya Gumanga kutumia mafunzo waliyoyapata ya namna ya kupata msaada wa sheria kwaajili ya kujipatia haki katika masuala mbalimbali.
Ameyasema hayo Januari 18, 2024 katika Mkutano wa hadhara wa kuhitimisha siku 10 za kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia wilayani Mkalama mkoani Singida.
‘’ Nimefurahishwa kwa namna mlivyoipokea kampeni hii na kujitokeza kwa wingi ili muweze kupata elimu juu ya masuala ya kisheria nawasihii muitumie elimu hii kujua haki zenu ‘’ Alisisitiza Ded Messos
Pamoja na hayo Bi.Messos amesema lengo la serikali ya awamu ya Sita kuleta kampeni ya msaada wa kisheria ni kuhakikisha wananchi wanapatiwa ufumbuzi wa changamoto zao nakuzijua sheria mbalimbali zinazohusu Ardhi, haki ya ndoa haki ya watoto pamoja na zinginezo na kuweza kupata haki .
Awali akiwasilisha mada inayohusu sheria ya Ardhi, Afisa Ardhi Wilaya ya Mkalama Protas Majumba amesema kuna sheria ya ardhi ya jumla,Vijiji na hifadhi huku akisisitiza kila Ardhi inasheria yake hivyo ni muhimu wananchi kutambua sheria hizo ili inapotekea changamoto wajue ni wapi wanaweza kupata haki zao.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.