Afisa Mifugo wilaya ya Mkalama Bw. Elias Mbwambo amesema kuwa zoezi hilo linaendelea katika kata ya Iguguno kwa Vijiji vya Iguguno na Senene na lilianza tar 19/10 /2022 hadi sasa takribani Ng’ombe 2,458 , Mbuzi 373 ,Kondoo 172 na Punda 49 wamekwisha tambuliwakwa kuvishwa hereni za Kielektroniki.
Aidha Bw. Mbwambo aliongeza kuwa utambuzi huu ni nyenzo muhimu katika uzalishaji wenye tija na faida kwa mifugo na mazao yake katika masoko ya ndani na nje ya Nchi ukilinganishwa na hapo awali ambapo mifugo ilikuwa inapigwa chapa kupata changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na mifugo iliyowekewa alama kufutika pia alama hizo kuharibu ubora wa ngozi kwakuwa na vidonda hivyo kukosa soko.
Hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi na wafugaji wote kupeleka mifugo ya kwaajili ya kutekeleza takwa hilo la kisheria kwani watapata faida nyingi ikiwa ni pamoja na kudhibiti wizi wa mifugo, kuuuza mifugo yao ndani na nje na Nchi pia itasaidia wao kupata mikopo na kuweza kufanya shughuli mbalimbali husuasani za kuongeza kipato chao.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.