Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe.Halima Omari Dendego leo ametembelea hospitali ya wilaya ya Mkalama pamoja na ujenzi wa Barabara ya kuelekea ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mkalama katika ziara yake ya kujitambulisha kwa Watumishi, Madiwani na viongozi mbalimbali wa serikali wilayani Mkalama.
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi hiyo, Mhe. Halima Omari Dendego ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, TARURA pamoja na kuwataka watumishi wa hospitali ya wilaya ya Mkalama kutunza vifaa tiba vinavyotolewa na serikali.
“Nimepita Majengo yote katika mkoa huu, kazi iliyofanyika hapa ni kazi iliyotukuka, hasa hili jengo. Hongereni sana. Wito wangu tutunze sana hivi vifaa. Lakini tuzingatie pia usafi” Mhe. Halima Dendego
Aidha mkuu wa mkoa ameutaka uongozi wa hospitali ya wilaya ya Mkalama kuhakikisha inaushirikisha uongozi wa wilaya, mkoa katika kufanya kampeni ya ukusanyaji damu safi na salama.
“Tushirikisheni katika programu ya kutafuta akiba ya damu, ukiona imepungua unamuita Mkuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa, Mwenyekiti wote tunaenda kukusanya damu” Mhe. Omari Dendengo
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.