Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida ikiongozwa Mhe.Martha Mlata, leo tarehe 11 Juni, 2025, imefanya ziara ya kukaguautekelezaji wa mradi mkubwa wa umwagiliajiunaotekelezwa na Serikali katika Kijiji chaIshinsi, wilayani Mkalama.
Mradi huo una thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 34 na unatarajiwakunufaisha zaidi ya wananchi 12,000kutoka vijiji vya Ndurumo, Msingi, Kidi naIshinsi, kwa kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo nakuinua uchumi wa kaya.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Martha Mlata ametoa wito kwa vijanakuendelea kuwa walinzi wa amani ya nchi na kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025, kwa utulivuna uzalendo.
“Amani ni msingi wa maendeleo ya taifa. Vijanamuendelee kuwa walinzi wa amani, msikubali kudanganywa. Oktoba mwaka huu,mjitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu,” amesema Mhe.Mlata.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Omary Dendego,amewahimiza vijana kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili, huku akiwatakawazazi kuendelea kuwasimamia vijana wao ili wawe raia wema, wachapa kazi, nawenye mchango chanya kwa taifa.
Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM ililenga kufuatiliautekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali pamoja nakusikiliza changamoto za wananchi, kwa lengo la kuhakikisha mipango yamaendeleo inakwenda sambamba na mahitaji halisi ya jamii.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.