Zao la pamba limetaja kuwa zao la Kimkakati na likilimwa kwa kufuata sheria na taratibu linaweza kuongeza pato la Taifa, Mkoa , Wilaya na kwa Mtu mmoja mmoja.
Balozi wa zao la pamba Kitaifa Agrey Mwanry amesema hayo Oktoba 2 wakati wa ufunguzi wa kampeni ya kuhamasisha kilimo cha zao la pamba katika wilaya ya Mkalama.
Katika ufunguzi wa kampeni hiyo alianza kufanya kikao cha ndani na wataalamu wa kilimo pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali , Watendaji wa Kata, Makatibu Tarafa , Wadau wa kilimo cha pamba , Viongozi wa AMCOS katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mkalama na ambapo Kampeni hiyo iliendelea katika Kijiji cha Kinyangiri na Lyelembo vilivyopo Kata ya Kinyangili.
Balozi Mwanry alitaja faida za zao la pamba kama likilimwa kwa tija na kimkakati kuwa litaongeza uzalishaji kutoka kilo 100- 250 ambao wakulima wanapata sasa kwa heka Moja na kufikia Kilo 2500 kwa heka moja.
Pamoja na hayo Balozi Mwanry alieleza kanuni mbalimbali za kilimo cha pamba ikiwa ni pamoja na kuandaa shamba kwa wakati , kupanda kwa wakati na kwakutumia vipimo stahiki cha Rula mbili kati ya shimo na shimo na rula moja kati ya Mbegu na mbegu , kupalilia kwa wakati na kufuata hatua za kupalilia , kuvuna kwa wakati pia kuchoma masalia ya mazao ambapo yasipo chomwa yanapelekea kuzalisha wadudu wanaoshambulia zao hilo pia aliwataka kunyunyiza dawa kwa wakati.
‘’Ninawashauri Wananchi kutumia fursa hii adhimu ambayo imekuja kwenu Mkalama fursa hazitolewi f ursa zinachukuliwa ‘’. Aliongeza Balozi Mwanry.
Baadhi ya wananchi wameishukuru Serikali kwa fursa hiyo na kuahidi watafuata sheria na kanuni za kilimo bora ili kuongeza tija katika uzalishaji wa zao la pamba wilayani Mkalama.
Ziara hii inaendelea leo Oktoba 3 katika Kata ya Mwangeza.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.