Imeelezwa kuwa mpango wa matumizi bora ya Ardhi ya kijiji ndio suluhisho sahihi la kuzuia matumizi yasiyo endelevu ya raslimali ya Ardhi .
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gumanga Mhe. James Mkwega wakat i akikabidhi hati za umiliki wa kimila Mia Tisa (900) Oktoba 28 2022 katika Kata ya Mpambala Wilayani Mkalama.
‘’Tunajua kuwa kumekuwepo migogoro mingi ya umiliki wa matumizi ya ardhi katika maeneo yenu kwa sababu mbalimbali ikiwepo wananchi kutokuwa na hati miliki za Ardhi , hali hii imepelekea wananchi kutumia muda mwingi kuhangaikia masuala ya kesi za umiliki wa ardhi badala ya kutumia muda huo katika kufanya shughuli za kujiongezea kipato’’ Aliongeza Mhe. Mkwega.
Aidha Mhe. Mkwega alisema zoezi hili niendelevu n hivyo kuwasihi wananchi kuheshimu na kufuata mpango wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao.
Mratibu wa mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula Kitaifa Bw. Joseph Kihaule aliongeza kuwa miongoni mwa maeneo yanayolengwa na mradi huu katika zoezi la kugawa hatimiliki za kimila katika wilaya ni pamoja na msitu wa Munguli uliopo kata ya Mwangeza kuuandaa kuutumia katika biashara ya hewa ya ukaa itakayopelekea kukua kwa pato la jamii ya Wahadzabe na Wilaya kwaujumla.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti baadhi ya wananchi wa Vijiji vya Mpambala, Mkiko, Nyahaa na Lugongo wameishukuru serkali kupitia ofisi ya Makamu wa Rais ( Mazingira ) kwa kugawa hati hizo kwao na kuongeza kuwa ugawaji wa hati hizo utaharakisha maendeleo yao na kuchochea kukua kwa uchumi.
Mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa Chakula kwemye maeneo kame unatekelezwa kwa Halmashauri ya Nzega iliyo Mkoa wa Tabora , Magu (Mkoani Mwanza) Kondoa ( Mkoani Dodoma), Mkalama ( Mkoani Singida ) na Micheweni (Pemba).
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.