Katika kuelekea maadhimisho miaka 61 uhuru wa Tanganyika wilaya ya Mkalama ni miongoni mwa Wilaya zinazojivunia mafanikio mbalimbali yatokanayo na uhuru huo katika Nyanja mbalimbali.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Afisa Mazingira wa wilaya Amon Sanga ameyataja mafanikio ambayo yamepatikana ndani ya Wilaya tangu uhuru ambayo yamegawanyika katika nyanya mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya , Elimu , miundombinu ya maji , Mawasiliano , Kilimo pamoja na umeme.
Sanga alisema kupatakana kwa Wilaya ya Mkalama kumerahisisha kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa Wananchi jambo ambalo ni mafanikio makubwa kwa Wilaya tangu uhuru.
‘’ tunajivunia miaka 61 ya uhuru kwani tumefanikiwa kupata Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya na kupata wilaya mpya kutoka wilaya Mama ya Iramba. Alisema Sanga
‘’Pia tunajivunia maboresho makubwa katika sekta ya Afya, tumepata Zahanati, Vituo vya Afya , Barabara, Maji , Umeme na mambo mengi ambayo kabla ya uhuru ilikuwa hamna’’. Aliongeza Sanga
Aidha Afisa mazingira huyo aliongeza kwakuwataka Wananchi kuwa wazalendo na kushiri katika shuguli mbalimbali za maendeleo pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita ambayo imeendelea kutoa fedha kwaajili ya maendeleo ya Wananchi.
Maadhimisho ya miaka 61 Uhuru mwaka 2022 kwa Mkoa wa Singida yatafanyika katika Kata ya Iguguno Wilayani Mkalama na Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ni ‘’MIAKA 61 YA UHURU AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU’’
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.