Katika kuelekea kilele cha wiki ya kichaa cha Mbwa duniani, Zaidi ya Mbwa Mia tatu na Hamsini (350) wamepatiwa chanjo ya kichaa cha Mbwa katika Vijiji vya Maziliga na Nduguti Kata ya Nduguti wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.
Zoezi hili limefanyika kuanzia tar 25 katika Kijiji cha maziliga na kumalizika Mapema leo September 26, 2021 Kijiji cha Nduguti katika Ofisi ya Kijiji cha Nduguti Ambapo Wafugaji wamesisitizwa Kupeleka Mbwa wao kupatiwa Chanjo ili kuwakinga na madhara yatokanayona ugonjwa huo pindi Mbwa wao wanapopata ukichaa.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali Linalojihusisha na usitawi wa Wanyama (Education for African Animals Walfare) Bwana Ayubu Nnko Amesema kuwa Jamii ione Umuhimu wa Kuchanja Mbwa wao ili kuepusha hasara zitakazowapa pindi Mbwa wao wanapopata ugonjwa na kung’ata Binadamu, Ambapo ametaja kwa nchi za Afrika na Tanzania ikiwemo kuwa kila mwaka hutumia Zaidi ya Dolla milioni ishirini kutibu watu waliopata ugonjwa wa kichaa cha Mbwa.
“Shirika la Education for Animals Walfare Tumekuwa tukishirikiana na Wilaya ya mkalama Tangu Mwaka 2019 ambapo kulikuwa kunaripotiwa matukio ya mara kwa mara ya mlipuko wa ugonjwa wa kichaa cha Mbwa , na Tanzania huungana na Dunia nzima kuazimisha chanjo ya Kichaa cha Mbwa kwa mwezi Septemba na Kilele chake huwa ni Septemba 28 kwa kila mwaka hivyo niwasihi wafugaji kutumia fursa hii adhimu kuleta Mbwa wenu wapate chanjo na chanjo hii inatolewa bure. ” Ameongeza Ayubu Nnko Mkurugenzi(EAAW).
Afisa mifugo wilaya ya Mkalama Bw. Dotto Michael ameishukuru Serikali kupitia Shirika la Education for Animals Walfare(EAAW) kuleta chanjo kwa wilaya ya mkalama tena bure kwaajiri ya kuchanja Mbwa hivyo kuwataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kuleta Mbwa kupatiwa chanjo ili kuunga mkono juhudi za serikali.
Aidha Bw Michael ameongeza kuwa zoezi hilo limesaidia kupunguza Ugonjwa wa Mlipuko wa kichaa cha Mbwa kutoka 8% kwa mwaka 2019 hadi kufikia 4% kwa mwaka 2020/2021 kwa wilaya ya Mkalama na ambapo amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na kwa mwaka 2021/2022 wanatarajia kufikia 2% ya kupunguza mlipuko wa Kichaa cha Mbwa.
Daudi Samsoni na Saimon Willium ni miongoni mwa wafugaji wa Mbwa ambapo wameishukuru serikali kuona haja ya kuwapelekea chanjo kwenye maeneo yao na kutoa chanjo hiyo bure kuwa ni fursa ya kipekee ambapo wameahidi kuwalinda na kuwatunza Mbwa wao vizuri kwakuwapa chakula na kuwajengea mabanda mazuri kwani Mbwa ni Rafiki wa Binadamu na Askari wazuri wa Nyumbani.
Kilele cha maadhimisho ya Kichaa cha Mbwa ni September 28.2021 huku kauli mbiu ikiwa ni “CHANJA MBWA WAKO NA PAKA WAKO MARA MOJA KWA MWAKA KUDHIBITI KICHAA CHA MBWA,KUMBUKA UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA HAUNA TIBA”.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.