Maafisa elimu Sekondari Wilaya ya Mkalama leo Januari 08, 2024 wametembelea shule baadhi ya Shule za Sekondari Wilayani hapa ili kujionea hali ya uandikishwaji ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2024.
Akiongea kwa niaba ya Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Mkalama Mwl Steven Ludovic ambaye ni Afisa Elimu taaluma Sekondari amesema kuwa Wilaya ya Mkalama inatarajia kupokea wanafunzi 4545 wa kidato cha kwanza ikiwa Wavulana ni 1909 na Wasichana 2636 lakini hadi sasa ni wanafunzi 303 pekee ndio wameripoti ikiwa Wavulana ni 118 na Wasichana 185 sawa na asilimia 6.7.
Pamoja na hayo Mwl Ludovic ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi kuendelea kuwapeleka wanafunzi kujisajili na kuanza masomo ya kidato cha kwanza kwani masomo yameanza mapema leo.
‘’ Nitumie fursa hii kuwataka wazazi mkawaandikishe wanafunzi ilinwasipitwe na masomo , tayari leo wameanza masomo ya’ English course ‘ kwahiyo msiwacheleweshe watoto ili wapate masomo ya awali yatakayowapa urahisi wa kuelewa Kiingereza watakapoanza masomo yao rasmi’’ Amesisitiza Mwl Ludovick.
Shule walizotembelea ni Shule ya Sekondari Nduguti, Mkalama One pamoja na Gunda Sekondari
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.