Katibu Tawala Wilaya Ya Mkalama Bi. Happyness Sulle ametoa wito wa watumishi wa afya wilayani Mkalama kutumia majukwaa mbalimbali kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupeleka watoto wao kupatiwa chanjo ili kukabiliana na maradhi mbalimbali yanaweza kuleta madhara kwa watoto kama vile vifo na hata ulemavu wa kudumu
Wito huo ameutoa Aprili 23,2025 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama wakati wa kikao cha Kamati ya Afya Ya Msingi Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama kujadili namna ya kufanikisha nyongeza ya dozi ya pili IPV2 ya chanjo ya polio itakayoanzia mwezi Mei,2025
"Nawasihi twendeni tukatoe elimu kwa wananchi, tutumie majukwaa mbalimbali, tushirikiane na viongozi wa dini katika kuelemisha wananchi umuhimu wa kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo ya polio" DAS Sulle
kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya Ya Mkalama, Dkt. Solomon Michael ametoa rai kwa viongozi wa dini pamoja na wadau wa afya wilayani Hapa kuhamasisha wananchi kujiunga katika mifuko ya bima ya afya ili kupunguza gharama za matibabu
Aidha, akiwasilisha taarifa kuhusu matibabu ya bure kwa wazee na watoto, Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Rehema Msawanga amesema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari -Machi 2025, jumla ya wazee na watoto 13727 wamepatiwa matibabu bure, ambapo watoto ni 11605 na wazee ni 2122
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.