• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Watendaji wa Kata Mkasimamie mikataba ya Lishe.

Imewekwa kwenye: January 29th, 2022


Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Sophia Mfaume Kizigo amewataka watendaji wa Kata kuhakikisha wanafuatilia Kwa ukaribu taarifa kwa wahudumu ngazi ya jamii kuhusu hali ya lishe Kwa watoto na afya ya Mama na mtoto ili kupata takwimu sahihi ya hali ya lishe wilayani hapa.


Amesema hayo wakati wa kikao cha tathimini ya mikataba ya lishe, jiongeze tuwavushe salama  na bima ya afya iliyoboreshwa Kwa robo ya pili ya Oktoba - Disemba Kwa mwaka 2021-2022.


Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ambapo amesema kuwa watendaji wanapaswa kushirikiana na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika kukusanya taarifa ya Hali ya lishe wilayani hapa kwani kwakufanya hivyo itapelekea Wilaya kufanya vizuri katika masuala ya lishe na afya ya Mama na mtoto na kupandisha   Kata zingine ambazo zimekuja hazifanyi vizuri.


"Niwashukuru watendaji Kwa mahudhurio yenu na kuwa watulivu katika kikao hiki ninachotaka kuwasisitiza ni kuhakikisha taarifa za kila Kata zinawasilishwa Kwa wakati pia nawaomba mshirikiane kuhakikisha Kata zenye kadi alama nyekundu zinafanya vizuri maana sisi ni wamoja na tunaifanya kazi Moja ya kuijenga Mkalama yetu". Aliongeza Dc Kizigo.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos amesema kuwa kucheleweshwa Kwa taarifa ndio sababu ya Kata nyingine kushindwa kufanya vizuri  ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka watendaji kuhakikisha Mkataba wa lishe unafanywa Kwa usahihi Katika Kata zote.


Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mkataba wa lishe Kwa Kata 17  kwaniaba ya Afisa lishe Wilaya ya Mkalama Bi. Jennifer Moses ameeleza watoto waliofikiwa na upimaji hali ya lishe na kupata  watoto wenye alama ya njano, alama nyekundu na alama ya kijani katika Kata husika ambapo ameshauri Elimu iendelee kutolewa Kwa jamii ili kujua umuhimu wa lishe pamoja na vyakula vinavyoshauriwa Kwa watoto pamoja na wanawake wajawazito.


Juliet Shirima Afisa lishe kutoka Action against hunger amesema  Hali ya kaya zilizojisajiliwa kwenye bima ya afya iliyoboreshwa (iCHF) kuwa hairidhishi Kwa Wilaya ya Mkalama na kushauri kuwa Kwa walengwa waliopata mbegu za mazao kutoka Action against hunger wakivuna wauze hata gunia Moja ili kuweza kupata fedha ya kujiunga na iCHF.


Sanjari na hayo Katibu wa afya Wilaya ya Mkalama Bw. James Ndimbo ametumia kikao hicho kuwataka wananchi kuona umuhimu wa kula makundi matano ya chakula pamoja na mazoezi huku akiwataka kina Baba kuambatana na wenzio wao pindi wanapopata ujauzito kwani kwakufanya hivyo itapunguza vifo vya Mama na mtoto .

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.