Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Sophia Mfaume Kizigo amewataka watendaji wa Kata kuhakikisha wanafuatilia Kwa ukaribu taarifa kwa wahudumu ngazi ya jamii kuhusu hali ya lishe Kwa watoto na afya ya Mama na mtoto ili kupata takwimu sahihi ya hali ya lishe wilayani hapa.
Amesema hayo wakati wa kikao cha tathimini ya mikataba ya lishe, jiongeze tuwavushe salama na bima ya afya iliyoboreshwa Kwa robo ya pili ya Oktoba - Disemba Kwa mwaka 2021-2022.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ambapo amesema kuwa watendaji wanapaswa kushirikiana na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika kukusanya taarifa ya Hali ya lishe wilayani hapa kwani kwakufanya hivyo itapelekea Wilaya kufanya vizuri katika masuala ya lishe na afya ya Mama na mtoto na kupandisha Kata zingine ambazo zimekuja hazifanyi vizuri.
"Niwashukuru watendaji Kwa mahudhurio yenu na kuwa watulivu katika kikao hiki ninachotaka kuwasisitiza ni kuhakikisha taarifa za kila Kata zinawasilishwa Kwa wakati pia nawaomba mshirikiane kuhakikisha Kata zenye kadi alama nyekundu zinafanya vizuri maana sisi ni wamoja na tunaifanya kazi Moja ya kuijenga Mkalama yetu". Aliongeza Dc Kizigo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos amesema kuwa kucheleweshwa Kwa taarifa ndio sababu ya Kata nyingine kushindwa kufanya vizuri ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka watendaji kuhakikisha Mkataba wa lishe unafanywa Kwa usahihi Katika Kata zote.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mkataba wa lishe Kwa Kata 17 kwaniaba ya Afisa lishe Wilaya ya Mkalama Bi. Jennifer Moses ameeleza watoto waliofikiwa na upimaji hali ya lishe na kupata watoto wenye alama ya njano, alama nyekundu na alama ya kijani katika Kata husika ambapo ameshauri Elimu iendelee kutolewa Kwa jamii ili kujua umuhimu wa lishe pamoja na vyakula vinavyoshauriwa Kwa watoto pamoja na wanawake wajawazito.
Juliet Shirima Afisa lishe kutoka Action against hunger amesema Hali ya kaya zilizojisajiliwa kwenye bima ya afya iliyoboreshwa (iCHF) kuwa hairidhishi Kwa Wilaya ya Mkalama na kushauri kuwa Kwa walengwa waliopata mbegu za mazao kutoka Action against hunger wakivuna wauze hata gunia Moja ili kuweza kupata fedha ya kujiunga na iCHF.
Sanjari na hayo Katibu wa afya Wilaya ya Mkalama Bw. James Ndimbo ametumia kikao hicho kuwataka wananchi kuona umuhimu wa kula makundi matano ya chakula pamoja na mazoezi huku akiwataka kina Baba kuambatana na wenzio wao pindi wanapopata ujauzito kwani kwakufanya hivyo itapunguza vifo vya Mama na mtoto .
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.