Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mosses Machali ametoa mwezi moja kukamika kwa mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST) miradi inayohusisha ujenzi wa miundo mbinu ya Shule za Awali na Msingi Wilayani hapa.
Mhe. Machali ametoa agizo hilo mapema leo April 5, 2023 katika ukumbi wa Sheketela uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama katika kikao kazi na Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa , walimu wakuu Pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo.
‘’Ninatoa mwezi mmoja baada ya vifungu vya fedha za utekelezaji wa mradi wa ‘Boost ‘ kusoma kwakweli sitokuwa na utani na mtumishi mzembe katika hili ninataka miradi hii ikamilike kwa wakati na tena kwa viwango’’ Alisisitiza Mhe. Machali.
Pamoja na haya amewataka wasimamizi wa Miradi hiyo kuhakikisha wanatafuta mafundi wa kutosha ili kuongeza kasi ya ukamilishaji wa miradi hiyo huku akiwataka kusitisha mara moja mikataba na mafundi wazembe watakaopelekea ucheleweshaji wa ujenzi huo Pamoja na kusimamia vizuri sheria za manunuzi ya vifaa vya ujenzi .
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bw. Selemani Msunga ambaye pia ni Afisa Kilimo,uvuvi na Mifugo amesema kuwa Wilaya imepokea shilingi Million 925,400,000/= kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 12 kwa Shule za Msingi Irama,Ishenga,Kikhonda,Kinyambuli, Ndala Pamoja na Nyahaa Pamoja ujenzi wa matundu 13 ya vyoo katika Shule hizo.
Aidha Bw. Msunga aliongeza kuwa watahakikisha wanasimamia vizuri fedha hizo na kuahidi kukamilisha miradi hiyo kwa wakati Pamoja na kuwachukulia hatua watumishi wote wazembe watakao jaribu kukwamisha zoezi hilo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.