Elimu ya chanjo ya UVIKO 19 inayoendelea kutolewa wilayani Mkalama imezaa matunda baada ya wananchi wapatao 2728 kupatiwa chanjo hiyo.
Mratibu wa chanjo wilaya ya Mkalama Bw. Duncan Kifaluka amesema kuwa wananchi wamepokea elimu na na kuunga mkono hatua iliyofikiwa na serikali ya kutoa mafunzo kwa ngazi ya taifa hadi kuwafikia wananchi walipo ya kuwa wamepokea zoezi hilo kwa mtazamo chanya na kuchukua hatua ya kupatiwa chanjo.
‘’sisi kama Wilaya tulipokea dozi 3550 na kufikia sasa zimetumika Dozi 2940 ambayo imefanya jumla ya Wananchi 2728 kupatiwa chanjo na hadi kufikia leo tumebakiwa na dozi 610 tu na zoezi bado linaendelea “Ameongeza Bw. Kifaluka mratibu chanjo.
Katika hatua nyingine ameeleza kuwa jitihada hizo zimesaidia jamii ya Wafugaji , wakulima na wawindaji ya Wahadzabe Kutoka Kijiji cha Munguli na Vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ambapo amesema takribani Wananchi mia moja(100) mpaka jana tar 7 /10 /2021 walipatiwa chanjo huku akisema zoezi hilo bado linaendelea .
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali na Serikali zamitaa (TAMISEMI) Idara ya jamii na Lishe Dinah Atinda ameeleza namna serikali inavyofanya jitihada za kupambana na janga la Corona na kuona umuhimu na kutoa elimu kwa jamii ili kila mtu aone umuhimu wa kuchanja kuepusha madhara makubwa zaidi .
Richard Magodi kutoka Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto ambaye alikuwa miongoni mwa waliofika katika Kitongoji cha Kipamba Kijiji cha Munguli kata ya Mwangeza kutoa elimu juu ya chanjo,ameeleza namna alivyofurahishwa na muamko na Mapokezi ya jamii hiyo kupokea zoezi la chanjo vizuri na kujitokeza kwa Wingi kupatiwa Chanjo ambapo ameeleza hii itasaidia kupunguza Vifo kwa Nchi na maeneo yote Duniani .
Miongoni mwa wananchi wa jamii ya Wafugaji , Wakulima na Wawindaji ya Wahadzabe Bw Edward Mashimba na Doricas James kutoka Kitongoji cha Kipamba wamesema kuwa wamepokea chanjo kwa mikono miwili na maelekezo yote yalitolewa na serikali na kujitokeza kupata chanjo ili wao wabaki salama huku wakiwashauri wengine wenye Imani potofu kuhusu chanjo hiyo kwenda kuchanja ili kulinda maisha yao na jamii kwa ujumla.
Kampeni ya Chanjo ya UVIKO 19 Ilizinduliwa Oktoba Mosi mwaka huu na Litaendelea hadi Oktoba 14 mwaka huu.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.