Jamii imetakiwa kuendelea kupokea miradi inayotolewa na serikali na kuunga mkono juhudi hizo kwakujitoa nguvu kazi zao katika kusaidia miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kuleta tija katika jamii.
Hayo yamesemwa Februari, 4 2025 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhe. James Mkwega katika ziara ya kamati ya Mipango na Fedha na Utawala ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo inayoendelea katika maeneo mbalimbali Wilayani hapa.
‘’Niwaombe ndugu zangu wananchi tuendelee kuunga mkono juhudi za Serikali kwakujitoa nguvu zenu ili miradi hii ilete tija’’ Alisisitiza Mhe Mkwega
Aidha kamati hiyo imeridhishwa na utekelezwaji wa miradi unavyoendelea ambapo walitumia fursa hiyo kuwapongeza wasimamizi na kuwataka kuongeza kasi kwenye miradi inayoendelea ili ianze kutumika kwa wakati muafaka.
Katika hatua nyingine Mhe. Mkwega amewataka wazazi kuwapeleka watoto shule kwa wingi kutokana na Serikali kuboresha miundo mbinu ya kujifunza pamoja na kuchangia chakula shuleni ili watoto wawe nautulivu na kupandisha kiwango cha ufaulu katika Wilaya , Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Sanjari na hayo baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye maaeneo ya miradi wameishukuru Serikali kwa miradi na kuahidi kushiriki kikamilifu ili kuunga mkono juhudi za serikali ambapo wameahidi kuilinda miradi hiyo kwa maslahi mapana ya jamii inayowazunguka.
Ziara hiyo ilianza kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mwalimu Shule ya Sekondari Mkalama One wenye thamani ya shilingi 95,000,000 .00 uliopo kijiji cha Maziliga Kata ya Nduguti,Ujenzi wa Madarasa matatu na matundu sita ya vyoo shule ya Msingi Mwandu Kata ya Iguguno wenye thamani ya shilingi 81,200,000.00 na baadaye ujenzi wa Bweni moja Shule ya Sekondari Tumuli Kata ya Tumuli wenye Thamani ya Shilingi 125,000,000.00
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.