• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI MKALAMA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Imewekwa kwenye: July 11th, 2024

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ndugu Godfrey Mzava amewataka wananchi wilayani Mkalama kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2024.

Wito huo ameutoa Julai 10,2024 mara baada ya kumaliza kukagua, kuzindua na kuweka jiwe la Msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali wilayani Mkalama.

“Uchaguzi upo tayari mlangoni, tujitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi huu muhimu wa kuchagua viongozi wetu. Tukio la kupiga kura halitachukua muda mrefu, twendeni tukapige kura. Lakini pia tulinde amani na umoja wakati wa uchaguzi,” Mzava

Akizungumzia suala la mabadiliko ya tabia nchi, Ndugu Godfrey Mzava amewataka wananchi wilayani Mkalama kuacha tabia ya kukata miti hovyo, badala yake wajikite katika upandaji miti ili kuepukana na madhara yanayotokana na uharibifu wa mazingira.

“Tuchukue wajibu wa kulinda mazingira yetu, nimepita shule ya Mkalama One nimeona kazi nzuri, nimeona mmeanzisha mradi wa mazingira. Tukifanya hivi tutakuwa vinara katika mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira” Mzava

Awali akizungumzia miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2024, Ndugu Godfrey Mzava ameipongeza wilaya ya Mkalama kwa usimamizi mzuri katika kusimamia fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo “Tumepita tumeona kazi kubwa imefanyika wilayani Mkalama, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu anatoa fedha lengo likiwa ni kuona wananchi wanapata huduma nzuri” Mzava

Mbio za Mwenge 2024 wilayani Mkalama zimezindua mradi mmoja na kuweka jiwe la msingi katika miradi miwili ambapo miradi yote ina thamani ya jumla ya shilingi 2,067,623,126.00 na umetembelea program 8 ambazo ni Lishe, Mazingira, Rushwa, Dawa za kulevya, VVU/UKIMWI, Malaria, Elimu kwa Mpiga Kura na Kongamano la Vijana.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.