• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali kwakufanya kazi kwa bidii na kutunza miradi ya Maendeleo.

Imewekwa kwenye: June 10th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt . Binilith mahenge ameishukuru serikali ya awamu ya Sita kutenga kiasi cha sh.2,118,079,899.00 kutoka  kwenye mfuko wa kimataifa wa mazingira katika kutekeleza mradi  wa kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula  katika kata ya Mpambala na Kata ya Mwangeza kijiji cha Munguli.


Amesema hayo  katika ziara aliyoifanya  wilayani hapa  ya kutembelea miradi  mbalimbali  ya maendeleo  inayotekelezwa  wilayani mkalama  katika kijiji cha  Singa kata ya Kinampundu na  kijiji cha Munguli kitongoji cha Kipamba  kata ya Mwangeza  na kusema  kukamilika kwa mradi hiyo itatatua changamoto nyingi za wananchi ikiwani pamoja na  kutatua kero za maji, na kutunza mazingira , kuzuia  mmomonyoko  kwenye  maeneo  yanayotekelezwa miradi.


Aidha amewataka wataalamu wa ngazi zote kusimamia vizuri pamoja  kushirikiana kutatua  changamoto  zitakazojitokeza ili kuharakisha maendeleo ya  Wananchi wa wilaya ya mkalama ikiwa ni pamoja na kutatua migogoro mbalimbali iliyopo katika maeneo  ya miradi.


Akitembelea bwawa la kijiji cha  Singa kata ya Kinampundu  lililochimbwa na wanufaika wa mradi wa kunusuru kaya masikini TASAF aliwataka wananchi hao kutumia mradi huo vizuri ili uweze kuwanufaisha kwakuwataka kulima kilimo cha umwagiliaji na kutoruhusu mifugo kuingia na kukanyaga   kujaza mchanga  kwenye  mradi ili maji hayo yaweze kudumu  hadi kipindi cha masika.


Awali akimkaribisha  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia  Kizigo alianza kwa kumshukuru Mkuu wa Mkoa kutembelea wilaya ya mkalama  kujionea maendeleo ya wilaya  na kuongeza kuwa  ziara yake inachochea kasi ya maendeleo kwani wananchi wanajisikia furaha kutembelewa na viongozi wa kubwa huku akimuomba Mkuu wa  mkoa Dkt . Mahenge inapotokea kugawanywa maeneo ya utawala na Kata ya Mwangeza iangaliwe kwa jicho la pekee kwani ni kubwa hivyo kupunguza ufanisi wa kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali.


Naye diwani wa kata ya Mwangeza  Mhe. Bosco  Samwel  aliongeza kuwa ni kweli serikali imefanya mambo makubwa katika kata yake na hasa kwa jamii ya Wahadzabe inayoishi  kijiji cha Munguli kitongoji cha Kipamba  lakini kilio  bado kipo kwenye ubovu wa miundo mbinu ya barabara , umeme, ukosefu wa  nyumba za walimu pamoja na uhaba wawalimu katika shule shikizi ya Kipamba ambayo tayari imesajiliwa pamoja na shule shikizi ya Mwasulagi ambayo hakuna barabara ya kufika katika shule hiyo.


Afisa mazingira wilaya ya Mkalama Bw. Amon Sanga alieleza utekelezaji wa mradi wa mazingira umesaidia kuwepo kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi  kwa vijiji vitano vinavyotekeleza mradi wa LDFS ,huku vikundi vya uzalishaji kiuchumi vikianza kunufaika na ufugaji kwa kupata mizinga ya nyuki  420 pamoja na kuwepo kwa msitu ambao tayari una hati miliki ya kimila unaotoa manufaa  mbalimbali  ikiwa ni pamoja na ufugaji wa nyuki, upatikanaji wa mahitaji ya  jamii ya kihadzabe kama vile dawa,mizizi , matunda na wanyama pori.


Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa TASAF mratibu wa TASAF wilaya ya Mkalma Bw. Gudluck Mlau alisema kuwa kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Mei  2022 Halmashauri ya wilaya ya Mkalama im epokea kiasi cha Tsh,.1,591,881,600.00 na malipo yamefanyika katika vijiji vyote 70 ambapo jumla ya walengwa 7,235 walinufaika na mradi huo huku kijiji cha Munguli kikipokea  fedha za ruzuku  kiasi cha Tsh.43,998,000.00 kwa kipindi cha mwezi  Januari  hadi Mei 2022 huku walengwa 354 wakipokea ruzuku zao kwa njia ya mtandao jambo linalowapa urahisi  wakupokea fedha zao .


Sanjari na hayo  Mratibu wa sensa wilaya ya Mkalama Bw.Daniel Tesha  alieleza maandalizi ya sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu kuwa yanaendelea vizuri na kuongeza kuwa  tayari  hamasa imeshafanyika kwa vijiji vyote70 vya wilaya ya Mkalama na tayari eneo  Maalumu limetengwa katika kitongoji cha Kipamba kijiji cha Munguli  maalumu kwa jamii ya wahadzabe na bajeti maalumu  imewasilishwa ofisi ya Takwimu taifa  ili jamii hiyo iweze kupata chakula katika siku hiyo ya sensa na kuweza kushiriki kikamilifu.


Baadhi ya wananchi wajamii ya wahadzabe wameishukuru serikali kuweka kipaumbele na kupeleka miradi mingi katika jamii hiyo huku wakiaahidi kuunga mkono  juhudi za serikali kwa kufanya kazi kwa bidii na kushiriki zoezi la sensa  ya watu na makazi ifikapo tar. 23 mwezi Agosti.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.