Wananchi wa vijiji vya Mwangeza, Munguli, Endasiku pamoja na Ikolo wameishukuru serikali ya awamu ya sita kupitia Bodi ya pamba Tanzania kuwapa elimu ya kilimo bora cha zao hilo inayolenga kuongeza tija katika uzalishaji na kupelekea kukuza vipato vyao.
Wamesema hayo mapema leo katika kampeni ya kuhamasisha zao la pamba kulimwa wilayani hapa kama zao la kimkakati .
Aidha wamesema mafunzo hayo yamekuja muda muafaka ambapo wakulima wa zao la pamba walikata tamaa , na kuongeza kuwa wamepokea maelekezo ya serikali na kuahidi kufuata utaratibu na njia bora za kilimo cha pamba ambapo hapo awali walikuwa wakitumia kilimo cha Kienyeji na kupelekea mavuno machache.
“ Tunaishukuru serikali inayoongozwa na Mama yetu mpendwa Rais Samia kumtuma Balozi wa zao la Pamba Nchini kufika kwenye maeneo yetu kuhamasisha kilimo cha pamba, chenye tija tutazingatia mafunzo haya maana hapo awali tulikua tunalima mashamba makubwa halafu tunapata mavuno kidogo’’ Ailiongeza Elias Mkilya miongoni mwa wakulima wa zao la pamba.
Pamoja na hayo wameiomba serikali kuwapa pembejeo kwa wakati ili waweze kujiandaa mapema na kuleta mapinduzi katika uzalishaji huku wakiomba pindi mazao yatakapo kuwa tayari wawe na uhakika wa soko ili wasikae na pamba kwa muda mrefu kwani wamelenga kujikwamua kiuchumi
Kampeni hii itaendelea kesho tar 04/10 katika Kata ya Ibaga wilayani Mkalama.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.