• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Wajumbe wa baraza la Ardhi na nyumba wilaya ya Mkalama kuunganisha familia zilizovunjika

Imewekwa kwenye: March 10th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dkt Binilith Mahenge amewataka wajumbe wa baraza la Ardhi na nyumba wilaya ya Mkalama kutumia hekima na busara  katika kutatua kesi zinazohusu migogoro ya Ardhi wilayani hapa Ili haki iweze kutendeka kwa wote.

Ameyasema hayo mapema leo wakati akiwaapisha wajumbe wa baraza la Ardhi na nyumba wilayani hapa katika ukumbi wa Sheketela uliopo halmashauri ya wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.

Dkt Mahenge amewataka wajumbe hao kusoma  nyaraka zote na kupitia mashauri yaliyotatuliwa na baraza lililopita ili kujifunza na sio kuanza kutatua kesi kabla ya kujifunza na  kuamua kwa matakwa yao .

" Mnakwenda kutatua kero za wananchi na  kero zilizo nyingi kwa wananchi Kimkoa , kiwilaya na Kata ni migogoro ya ardhi hivyo mkatumie hekima busara katika kutenda haki na msio chanzo cha migogoro" Aliongeza Dkt Mahenge Rc Mkoa wa Singida.

Pamoja na hayo aliwapongeza wajumbe hao kwa kuteuliwa kuwa wajumbe wa baraza hilo na kuwa miongoni mwa wachache waliopata nafasi hiyo kati ya wengi walioomba nafasi na kuwataka kufanya kazi kwa weledi na kushirikiana na mwenyekiti wa baraza la Ardhi wilaya katika  kutumikia wananchi.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo aliwataka wajumbe hao kuwa kiungo Cha kuunganisha familia zilizofarakana kutokana na migogoro ya ardhi Kwa kutenda haki kwa uadilifu Mkubwa huku akiwataka kutumia nafasi zao vizuri na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama  Mhe.James Mkwega amesema kuwa tukio hilo ni la kihistoria kwani toka kauanzishwa Kwa wilaya mwaka 2014 hakujawahi kuwa na baraza la Ardhi kitu kilichopelekea wananchi kukosa haki kwa kushindwa kufuata  huduma wilayani Iramba kutokana na umbali uliopo kutoka Mkalama hadi Iramba hivyo kuwataka wajumbe kutenda haki kwa kuzingatia taratibu na viapo  vyao.

Mwenyekiti wa baraza la Ardhi na nyumba wilaya ya Mkalama na Iramba Baraka shuma amesema kuwa baada ya mchakato kufanyika kuwapata wajumbe hao kilichofuata ni kula kiapo kwaajili ya kuanza majukumu yao huku akipongeza kupatikana kwao kwani itapelekea kurahisisha upatikanaji wa huduma wilayani Mkalama kwani wananchi wengi walipoteza haki zao kwakushindwa kufika wilayani Iramba kutokana na umbali na sababu zingine ikiwemo umri na kipato kidogo hivyo kupelekea haki zao kupotea.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia  Messos alieza mchakato  wa  maandalizi wa zoezi la kukusanya taarifa za Anuani za Makazi na Postikodi katika Wilaya ya Mkalama kuwa unaendelea vizuri na hadi kufikia Sasa tayari wameshapata majina ya vijana wazalendo 350 watakao fanya kazi hiyo ambapo walitumia watendaji wa kata kuwapata vijana hao waadilifu na wazalendo huku vijana waliohitimu mafunzo ya jeshi la akiba  wakipewa kipaumbele.

Sanjari na hayo amesema kuwa tayari elimu imetolewa Kwa wajumbe wa sensa ngazi ya kijiji na kitongoji ambapo watendaji wa kata walitakiwa kutambua makadirio ya Anuani za Makazi na tayari zoezi hilo limefanikiwa nakubaini Anuani za Makazi elfu arobaini na Tano (45,000) na wiki ijayo hamasa itaanza kutolewa kwa wananchi ya namna ya kushiriki katika zoezi la kukusanya taarifa za Anuani za Makazi na Postikodi pamoja na sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti Mwaka huu.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.