Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka jioni ya leo amevikabidhi vikundi 10 vya ujasiriamali hundi zenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 37.8 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mwongozo wa bajeti wa Serikali unayoitaka kila Halmashauri kutoa asilimia 10 ya fedha zake kuviwezesha vikundi vya wanawake na vijana mikopo ya riba nafuu.
Fedha hizo zimekabidhiwa kwenye vikundi 10, saba vya vijana na vitatu vya wanawake ambapo baada ya kukabidhi hundi hizo Mhe. Masaka alivitaka vikundi hivyo kuhakikisha vinatumia fedha hizo kufanyia shughuli za maendeleo ili viweze kupata faida na kurejesha fedha walizopewa ili watoe fursa ya vikundi vingine kukopeshwa kwa haraka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhandisi Godfrey Sanga alisema kuwa fedha Halmashauri hiyo itaendelea kutoa fedha zaidi kwa vikundi kulingana na ongezeko la mapato yake ya ndani.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.