MKUU wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amekutana na viongozi wa dini, machifu pamoja na Maafisa Tarafa kuongea kuhusu kulinda mmomonyoko wa maadili katika jamii pamoja na kudumisha Amani na mshikamano, taifa linapoelekea katika uchaguzi Mkuu.
Kikao hicho kimefanyika Mei 22, 2025 katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ambapo amewahimiza viongozi hao kuendelea kutoa elimu ya maadili katika jamii pamoja na kukemea vitendo vya ushoga na Usagaji ili kuwa na Taifa la watu wenye hofu ya Mungu.
‘’Nimewaita hapa viongozi wa dini zote na madhehebu yote, machifu , viongozi wa chama na Serikali, Maafisa Tarafa ili tuzungumze kuhusu maadili na malezi ya watoto katika jamii najua nyie mna sauti , nendeni mkapaze sauti zenu msikitini,kanisani na huko kwenye jamii kuhusu malezi ya watoto pamoja na kukemea vikali suala la ushoga’’ Amesisitiza Dc Machali.
Pamoja na hayo Mhe. Machali amewataka kudumisha Amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu na kuongeza kuwa usalama wa Nchi ni muhimu kuliko kitu chochote hivyo kuwasihi kuhubiri amani nyakati zote.
Hata hivyo hakusita kusisitiza maadili kwa watumishi wa umma ambapo amewataka kuwa mfano wa kuingwa katika jamii kwakufuata misingi na maadili ya utumishi ili jamii ijifunze kupitia wao.
Leonard Mtua, Mchungaji wa Kanisa la TAG Iguguno, Miraji Ibrahimu Shekhe wa Wilaya ya Mkalama pamoja na Hamisi Omary Chifu kutoka Tarafa ya Kinyangiri wameahidi kuunga mkono juhudi za serikali kwa kulinda maadili katika jamii na malezi ya watoto nakuongeza, kuhubiri Amani na utulivu wa Taifa nyakati zote.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.