Vijana wametakiwa kujitambua na kuthamini Maisha yao kwa kujikinga na maambukizi mapya ya VVU kwani ndio nguvu kazi ya Taifa.
Afisa Tarafa wa Tarafa ya Nduguti Bw. Remigius Ngole ameyasema hayo mapema leo katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani alipo mwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mkalama katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Gumanga Kata ya Gumanga Wilaya ya Mkalama.
‘’Vijana ni kundi linalokabiliwa na changamoto kubwa ya maambukizi mapya ya VVU Nchini na takwimu za maambukizi mapya ya VVU zinaonyesha kwamba 40% ya maambukizi yametokea kwa vijana na katika hao 80% ni vijana wa kike’’. Aliongeza Bw. Ngole
Hata hivyo aliongeza kuwa maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI miongoni mwa wanaume, Wanawake na Vijana wenye umri kati ya miaka 15-49 ni mkubwa .
Aidha aliongeza kwakusema Takwimu za mwaka 2022 kutoka January hadi Oktoba 2022 waliopimwa ni 17,273 ambapo Wanaume ni 6741 na Wanawake ni 10,532 kati yao 245 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU sawa na 1.4%, Wanaume walikuwa 78 sawa na 1.1% na Wanawake walikuwa 165 sawa na 1.5% huku Vijana wenye umri wa miaka 15-26 waliopimwa ni 1075 waliogundulika kuwa na maambukizi mapya ni 155 sawa na 1.4%.
Sanjari na hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhe. James Mkwega aliwataka wananchi kuwa na desturi ya kupima afya zao wakibainika wana maambukizi waanze kutumia dawa mapema ili kufubaza virusi na kuchukua tahadhari ya kuambukiza wengine.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ‘’MKALAMA BILA UKIMWI INAWEZEKANA, PIMA, JITAMBUE, ISHI, IMARISHA USAWA ‘’
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.