USHIRIKIANO UTALETA MATOKEO CHANYA KATIKA KUONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO MKALAMA' DC SAKULO MISENYI '
Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wamekamilisha ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Kagera yenye lengo la kutembele na kujifunza uwekezaji katika Sekta ya Viwanda, Kilimo pamoja na kujifunza namna ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ambayo wamejifunza katika Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi Mkoani humo.
Ziara hiyo ilianzia katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali, Wilson Sakulo amewataka kutumia ziara hiyo kuleta matokeo chanya katika Wilaya ya Mkalama , ambapo ametaja siri kubwa ya mafanikio ni ushirikiano baina ya Viongozi, Wataalamu pamoja na madiwani.
‘’ Ninapenda kuwahakikishieni wanamkalama kuwa hakuna muujiza mkubwa kama ushirikiano, mnatakiwa mkashirikiane baina ya viongozi wa Wilaya, Wataalamu pamoja na madiwani’’ aliongeza Kanali Sakulo
Aidha, Kanali Sakulo amewataka kusimamia vyanzo vya mapato walivyonavyo ili viweze kuleta mafanikio mazuri pamoja na kuongeza mapato ya Halmashauri ambapo pia aliwataka Waheshimiwa Madiwani kusimamia suala hili vizuri kwani wana muda mwingi wakukaa na wananchi kuwaambia umuhimu wa kulipa kodi kwa maslahi ya Wilaya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi Mhe. Projestus Tegamaisho aliongeza kuwa Halmashauri ya Misenyi kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 ilijipanga kukusanya kiasi cha Shilingi Bilion 4.255 lakini hadi kufikia June 30 mwaka huu walifanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 6.085 sawa na 125% ambapo alisema kuvuka malengo hayo yanachagizwa na ushirikiano mkubwa kati ya Madiwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi.
Pamoja na hayo Mhe.Tegamaisho aliongeza kuwa mafanikio hayo pia yanatokana na mikakati mbalimbali waliojiwekea katika kufikia malengo ikiwa ni pamoja na uwepo wa Doria za kila siku (mchana na usiku), kuwepo kwa Vizuizi katika maeneo maalumu ambayo wanakuwepo vibarua na mgambo pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara ambao ndio walipa kodi / Ushuru wa Halmashauri.
@ded_mkalama @missenyidc @ortamisemi @
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.