Imeelezwa kuwa upatikanaji wa Maji safi na salama katika kijiji cha Milade Kata ya Tumuli utapunguza migogoro ya familia inayosababishwa na wakina Mama kutumia muda mwingi kutafuta Maji badala ya kuhudumia familia zao .
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo amesema hayo July 28 wakati akikabidhi mradi na kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa Maji uliopo kijiji cha Milade Kata ya Tumuli.
"Sasa mmepata mradi wa Maji ,mradi huu utapunguza zile kero, mama anaamka asubuhi anamuacha Baba kalala kitandani anafuata Maji umbali mrefu muda huo Baba anahitaji chakula unarudi umechoka mwisho wa siku Baba anaanzisha ugomvi kwa kuchelewa kurudi" aliongeza Dc Kizigo.
Aidha Dc Kizigo aliutaka uongozi wa jumuiya za watumia maji kuhakikisha wanasimamia vizuri mradi na kuweka pesa benki zitokanazo na mauzo ya maji kuepuka usumbufu wakukaa na pesa mkononi kwani inaweza kuwapelekea kutumia kwa matumizi yao binafsi.
Hata hivyo aliwataka Wananchi kupokea mradi huo na kuutunza, kuchangia gharama za uendeshaji wa mradi kwa kununua Maji Kwa ujazo wa ndoo ya Lita 20 Kwa shillingi 40 na kuhakikisha wanatunza miundo mbinu ya maji kwa vizazi endelevu.
Katika hatua nyingine aliwataka Wananchi kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na Makazi Agosti 23 Mwaka huu kwakutoa taarifa sahihi za familia zao ikiwepo taarifa za wenye ulemavu kwenye familia Ili kurahisisha utekelezaji kwa Serikali kupanga mipango kulingana na mahitaji sahihi kwa makundi Maalumu.
Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Antidus Muchunguzi alisema kuwa mradi huo umegharimu Tsh. 502,000,000 na unatawanufaisha Wananchi wapatao 3060 wa kijiji cha Milade na kuongeza kuwa wamepokea maombi 100 ya kuunganisha Maji majumbani .
Mhandisi Muchunguzi Aliongeza kuwa kukamilika Kwa mradi huo utaongeza hari ya Upatikanaji Maji safi na salama Kwa asilimia 1.3 kiwilaya na kupelekea Wananchi kukua kiuchumi kutokana na kuwa na muda mwingi wa uzalishaji Mali .
Mhe .Bilali Msengi diwani wa Kata ya Tumuli aliishukuru Serikali kupitia Wakala wa Maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) kupeleka mradi wa Maji katika kijiji Cha Milade na kusema kuwa mradi huo utawanufaisha wananchi kwa kupata Maji safi na salama pia kupunguza Magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.
Pamoja na hayo ameahidi Kwa niaba ya wananchi kutunza miundo mbinu ya mradi huo na kuahidi kupanua mradi ili adha ya upatikanaji Maji safi na salama kuwa historia katika kijiji cha Milade na Kata ya Tumuli Kwa ujumla.
Mradi huo umehusisha ujenzi wa Tenki la Lita 90,000 kwenye mnara wa mita 9 nyumba ya mashine Moja (1) ulazazi wa mabomba km 11.39 pamoja na ujenzi wa vituo 12 vya kuchotea maji.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.