Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Mhe.James Mkwega amewataka Madiwani kushiriki pamoja katika kukusanya mapato kwa maendeleo ya Halmashauri na kwa taifa kwa ujumla. Wito huo ameutoa leo Mei 18,2024 wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2023/24 kilichofanyika katika ukumbi Sheketelea wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
"Uhai wa Halmashauri ni mapato, tunapata shida sana tunaposikia kata flani inalalamikiwa kutoresha ushuru. Sheria hizi tunazopitsha ni za kulinda mapato. Tuwaelimishe wananchi wetu tutii hizi sheria kwasababu tunajenga nchi yetu" Mhe. Mkwega
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.James Mkwega amewakumbusha watumishi kuepuka kujihusisha na masuala ya kisiasa na badala yake wajikite katika kufanya kazi kulingana na taaluma zao kwa ajili ya maendeleo ya wilaya na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi.Asia Messos amekumbusha Madiwani kuweka kipaumbele pia kukomesha suala la utoro kwa wanafunzi mashuleni.
“Changamoto ya utoro katika wilaya yetu imekuwa ukubwa, kwa leo nawaomba Madiwani walibebe suala hili katika ajenda zao ili kuhakikisha wanafunzi watoro wanapatikana” B.Asia Messos
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.