• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Tusiwaibie wakulima- Masaka

Imewekwa kwenye: April 13th, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe: Mhandisi  Jackson Masaka leo amefanya ziara ya kushtukiza katika kijiji cha  Dominic kwa ajili ya kukagua ujenzi wa soko la Vitunguu na kuchunguza ufungashaji wa vitunguu hivyo kwenye mifuko kabla ya kupelekwa sokoni ambapo amebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na wafanyabiashara wanapofika mashambani.

Akiwa katika shamba la Mkulima mmoja aliyejulikana kwa majina ya Richard isaya, Mhe: Masaka ameshuhudia mfanyabiashara mmoja akiwa anapakia vitunguu ambavyo ameviweka kwenye ujazo wa zaidi ya Kilo 130 kwa gunia kinyume kabisa na sheria na taratibu za ufungashaji wa mazao ya Vitunguu ambapo mnunuzi anapaswa kufungasha ujazo wa Kilo 100 hadi 105 kama vitunguu hivyo vitakuwa havijakauka vizuri.


Huu ndio ufungashaji alioukuta Mhe: Masaka baada ya kufika shambani hapo


“Sitaki kuingilia makubaliano ya bei mliyokubaliana lakini sipo tayari kuona Mkulima akikandamizwa kiasi hiki kwa sababu ametumia nguvu, fedha na muda mwingi  mpaka kufikia hatua ya kuvuna na pia utaratibu huu unaifanya halmashauri kupoteza mapato kwa kiasi kikubwa sana” Amesema Masaka.

Mhe: Masaka ameongeza kuwa kila mfanyabiashara anayeingia katika Wilaya ya Mkalama ni lazima afuate sheria ndogondogo na taratibu zilizowekwa katika Wilaya hiyo na kamwe asilinganishe taratibu za Mkalama na maeneo mengine kwa sababu kila Wilaya ina Mkuu wake wa Wilaya na ana utaratibu wake wa kuongoza.

Kufutia tukio hilo, Mhe: Masaka aliagiza vitunguu hivyo vitolewe kwenye mifuko hiyo na kupimwa upya katika ujazo unaokubalika kisheria  na mfanyabiashara huyo alipe ushuru hapo hapo shambani kabla hajasafirisha mazao yake.

Naye Meneja wa wakala wa Vipimo  Mkoa wa Singida, Bw. Albogast Kajungu amesema kuwa ufungashaji wa mazao kwa kutumia mifuko ya aina yoyote tofauti na gunia la katani ni kinyume na sheria na kutokana na mabadiliko ya sheria yaliyofanyika hivi karibuni kutenda kosa hilo hakumuweki hatiani mfanyabiashara pekee bali mpaka dereva anayesafirisha mazao  hayo.

“ Lakini pia wakulima waepuke kupima mazao yao kwa kutumia vifaa vya plastiki kama vile ndoo na visado kwa sababu vyombo hivyo vikipata joto hutanuka na kuongeza ujazo wa mazao jambo ambalo ni udanganyifu na kinyume na sheria ya ufungashaji mazao” Alimalizia Kajungu.

Ni kwa muda mrefu hivi sasa wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wamekuwa wakiwaruhusu wafanyabiashara kufungasha mazao shambani kwa kutumia nyavu huku wafanyabiashara hao wakidai kutumia chombo kingine kinyume na hapo kunawakosesha soko hasa wanaposafirisha mazao hayo katika nchi za jirani kama Kenya na Uganda.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.