Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Jackson Masaka amefanya ziara katika kata ya Iguguno ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kawaida kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Katika Ziara hiyo Mhe: Masaka aliambatana na Katibu Tawala wa Wilaya Bi. Elizabeth Rwegasira, Afisa Kilimo wa Wilaya bw. Cuthbert Mwinuka na watendaji mbalimbali wa Tarafa, Kata na Vijiji.
Moja ya mambo aliyoyafanya Mhe: Masaka mara baada ya kufika katika kata hiyo ni Kushiriki kupanda miche ya miembe ikiwa ni sehemu ya sera ya utekelezaji wa sera ya taifa ya utunzaji mazingira na uimarishaji wa lishe bora kwa wananchi ambapo aliwasisitiza wananchi wote wa kata hiyo kuhakikisha suala la upandaji miti linakuwa ni endelevu.
“Zoezi hili pia ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa ambapo kama tunakumbuka aliagiza kila kaya ni lazima ipande miche ya miembe pale inapokuwa na maji ya kutosha” Amesema Masaka.
Aidha Mhe: Masaka alitumia ziara hiyo kukagua na kupata maelezo kuhusu ujenzi wa madarasa ya kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Iguguno ambapo aliridhiswa na kasi ya ujenzi huo na kumsisitiza Mkandarasi kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo kwa wakati ili kuhakikisha shule inaondokana na changamoto ya uchache wa madarasa.
Katika ziara hiyo Mhe: Masaka alilazimika kuamuru Mwananchi Joseph Luther awekwe ndani kwa masaa 24 baada ya Mwananchi huyo kutoa lugha iliyoashiria uvunjifu wa amani kwa jamii huku pia akiwa na rekodi ya kusababisha vurugu mara kwa mara panapokuwa na mikutano ya hadhara.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.