Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Moses Machali ametoa wito kwa watendaji wa serikali wilayani Mkalama kutumia vizuri takwimu za Sensa ya watu na Makazi ya 2022 kuleta maendeleo kwa wananchi na kwa taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo ameitoa Mei 7,2024 wakati wa Mafunzo na Tathimini ya matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya 2022 kwa makundi mbalimbali yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheketela wilayani Mkalama
“Takwimu hizi zimetusaidia sana katika kupanga miradi ya maendeleo.Leo tumefahamu idadi ya watu katika wilaya yetu,watu 255,514. Tumieni takwimu hiz kuleta maendeleo kwa wananchi” Mhe.Machali
Naye Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Tanzania Visiwani (Zanzibar),Balozi Mohamed Haji Hamza amesema kuwa Sensa ya 2022 inamafanikio makubwa zaidi kulinganisha na Sensa zilizowahi kufanyika huku akiwashukuru wananchi kwa kufanikisha zoezi hilo.
“Wananchi mlifanikisha Sensa hii kwasababu mlielewa. Hongereni sana na asante sana. Mlifanya vizuri sana, Tujipongeze watanzania. Tumpongeze Rais Dkt Samia Suluhu Hassan” Balozi Mohamed Haji Hamza
Kwa upande wake, Mtakwimu Mkuu wa serikali Dkt. Albina Chuwa amewapongeza wananchi wa Mkalama kwa mtikio mkubwa wakati wa zoezi la Sensa na kuwaomba kuendelea kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa wakati wa ukusanyaji mbalimbali wa takwimu unaofanywa na serikali.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.