Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali ameziagiza Jumuiya za maji zilizo chini ya Mamlaka ya Maji RUWASA wilayani Mkalama kuhakisha zinatumia mapato yake kupeleka huduma za maji kwa wananchi. Kauli hiyo ameitoa Januari 17/2024 wakati wa mkutano wa nusu mwaka wa wadau wa sekta ya maji wilayani hapa uliofanyika katika hospitali ya wilaya ya Mkalama.
"Tujali fedha za serikali, tumieni mapato yenu kupeleka maji kwa wananchi. Kuna baadhi ya viongozi wa Jumuiya wanahujumu mapato. Achane kuhujumu mapato.Kila mwezi nataka taarifa za mapato sanjali na mipango ya kupeleka maji kwa wananchi. Wekeni utaratibu mzuri wa kuwasiliana na wananchi kuhusu taarifa mbalimbali" Mhe. Machali
kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Mkalama Mhe. Peter Masindi amewataka watumishi wa RUWASA kuwa waadilifu wakati kutimiza majukumu yao na kuacha kubambikia bili za maji wananchi sambamba na kuboresha huduma kwa wateja ili kuwa karibu na wananchi.
Awali akisoma taarifa fupi kuhusu hali ya upatikanaji maji safi na salama, Meneja RUWASA, Injinia Christopher Saguda amesema kwasasa hali ya upatikanaji maji katika wilaya ya Mkalama ni asilimia 68.23 ambapo zaidi ya wananchi 170 wameunganishwa na huduma ya maji kati ya wananchi wote 255,514 wa wilayani Mkalama kulingana na takwimu za sensa ya 2022
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.