Walimu wametakiwa kusikiliza kwa makini na kujifunza namna mtaala mpya utakavyoenda kufanya kazi ili kuwasaidia kuendana na ,mabadiliko ya mtaala huo utakaoanza kutumika mwaka huu kwa madarasa ya awali hadi la tatu .
Akiongea wakati akifungua mafunzo kwa walimu katika Shule ya Msingi Nduguti iliyopo Kata ya Nduguti , Wilaya ya Mkalama Mthibiti Mkuu ubora wa Shule Ignatus Kinyeje amesema kuwa mafunzo haya yakawe ni chachu ya kuleta mabadiliko katika taaluma huku akiwasihi walimu hao kuendana na mabadiliko hayo kwakuendelea kujifunza.
‘’Leo tunafungua mafunzo haya kwa naiaba ya mafunzo yote yanayoendelea leo Wilayani Mkalama ninawataka walimu kuwa na bidii katika mafunzo hayo pia mkipata fursa ya kusoma mkasomee masomo ya kifaransa na kichina kwani ndio yameongezwa katika mtaala huu mpya’’ Alisisitiza Kinyenje
Pamoja na hayo Mwl Kinyenje amewataka walimu hao kuwa na bidii katika ufundishaji katika kupandisha kiwango cha ufaulu wilayani hapa huku akiwataka kudhibiti suala la utoro kwa wanafunzi hususani katika kipindi hiki cha muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2024.
Naye Kaimu Afisa Elimu Msingi Mwl. Amina Irumba aliwataka walimu hao kuendana na mabadiliko ya Tekinolojia husani katika kipindi hiki cha kutumia (TEHAMA) shuleni na kutumia mifumo mbalimbali katika kurahisisha utendaji kazi ambapo amesisitiza kuwa makini na taarifa zao za siri.
‘’ Ninawaomba walimu tuwe makini na taarifa zenu maana sasa mnatumia mifumo katika utendaji kazi wenu , wengi wetu bado hatuja ‘master’ kutumia mifumo hiyo mnapoenda huko ‘Stationary’ kuweni makini na taarifa zenu za siri hususani kutoa Nywira zenu’’ Alisisitiza Mwl Irumba.
Aidha Mwl Irumba amewataka walimu kutumia vishkwambi walivyopewa kujisomea na kujifunza vitu mbalimbali kwaajili ya kuboresha utendaji kazi wao huku akiwaonya kuacha kutumia vishkwambi hivyo kwaajili ya kucheza michezo ya kubahatisha “ Kubet’
Sanjari na kuzindua mafunzo hayo timu hiyo ya Maafisa Elimu Wilaya pamoja na Uthibiti ubora Elimu Wilaya wamendelea kukagua hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza kwakutembelea Shule za Nduguti Shule ya Msingi, Gumanga, Ibaga, Mkalama pamoja na Shule ya Msingi Chemchem.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.