TUDUMISHE AMANI TULIYONAYO KWANI ILIGHARIMU UHAI WA MASHUJAA WETU' DAS MASINDI '
Katibu Tawala Wilaya ya Mkalama Peter Masindi leo( Julai 25 2023) ameongoza zoezi la usafi lilofanyika katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ikiwa ni kuunga juhudi za mashujaa waliopambana kwaajili ya Amani na uhuru wa Taifa la Tanzania.
Baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi Masindi alipata wasaa wakuongea na watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kuwakumbusha mambo mbalimbali ya kiutumishi
Pamoja na Haya Masindi aliwataka watumishi kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii na kuendelea kuilinda Amani ya Taifa hili ambalo lilipambaniwa na watu shupavu ambao iliwalazimu wengine kupoteza maisha yao kwa usalama na Amani ya Taifa hili.
Katika hatua nyingine Afisa Mliasili na uhifadhi wa mazingira Rodney Ngalanda na Afisa Elimu Sekondari Said Kalima wamesema kuwa Wilaya ya Mkalama inatambua na kuthamini mchango wa Mashujaa walioipambania Nchi na kuenzi siku hii muhimu kwakufanya usafi katika maeneo mbalimbali huku wakisisitiza vijana kuiga mazuri yaliyofanywa na mashujaa kwa maslahi ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.
MKALAMA DISTRICT COUNCIL
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.