MKUU wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge amelaani na kukemea vitendo vya wizi na mauaji Kwa waendesha Bodaboda ambayo Wamekuwa wakifanyiwa na mwisho kuporwa pikipiki zao na watu wasiojulikana.
Rc Mahenge amesema hayo jana wakati akitoa pole kwa wafiwa wa Iddi Hassan (25) mkazi wa Iguguno wilayani Mkalama mwendesha bodaboda ambaye aliuawa kwa chomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni na tumboni na mtu asiyejulikana ambaye alimkodi.
Aidha Rc Mahenge amewataka wananchi wa wilaya ya Mkalama na Mkoa Kwa ujumla kuchukua tahadhari kwa watu wasiowafahamu wanaofika kwenye maaeneo yao na kuwatilia mashaka kuchukua tahadhari ya kujilinda na kutoa taarifa Kwa vyombo vya ulinzi.
Akitolea mfano moja ya tukio lililotokea hivi karibuni Kata ya Nduguti wilayani hapa ambapo mtu mmoja aliyejitambusha kuwa amefika katika kata ya Nduguti kama muajiriwa wa Jeshi la Polisi ambaye alipanga katika nyumba moja ya kulala wageni akiwa na mwanamke aliyedai ni mke wake.
Amesema mtu huyu alikuwa akimtumia mwendesha bodaboda mmoja kumpeleka maeneo tofautitofauti na baada ya kuona amekwisha mzoea wakati wakinywa chai alimwambie amuachie pikipiki yake ili aende kuripoti kituo cha polisi kuhusu kuanza kazi ambapo alimruhusu kuondoka na pikipiki yake na kutokomea nayo kusikojulikana na walipoenda nyumba ya kulala wageni walimkuta na huyo mwanamke aliyedai ni mke wake amekwisha ondoka.
Hata hivyo Dkt. Mahenge amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha watu wote waliofanya tukio hilo watakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikulu ambacho alikuwa akiishi kijana huyo Christina Lema amesema wamesikitishwa sana na tukio hilo kwani marehemu alikuwa hana ugomvi na mtu yeyote na alikuwa akishirikiana na waendesha bodaboda wenzake kwenye shughuli zao.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.