• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Tatizo la Maji Mkalama litabaki kuwa historia-Kamwelwe

Imewekwa kwenye: September 29th, 2017

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Isack Kamwelwe ameuhakikishia uongozi wa Wilaya ya Mkalama kuwa kufikia mwaka 2020 tatizo la Maji litakuwa historia katika Wilaya hiyo.

Mhe. Kamwelwe ameyasema hayo mapema jana wakati wa ziara yake ya Kikazi Wilayani Mkalama ambapo pamoja na mambo mengine amefurahishwa na kasi ya maendeleo ya Wilaya hiyo huku akiwapongeza Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji, Mwenyekiti wa Halmashauri na Mbunge wa jimbo la Mkalama kwa ushirikiano mkubwa walionao katika kuhakikisha Mkalama inapiga hatua siku zote.

“Mbunge wenu amekuwa akiniomba sana nifike huku ili nijionee changamoto ya Maji  na nilimhakikishia kuwa ntakuja tena nashukuru nimekuja kipindi cha kiangazi ili nijionee hali ya upatikanaji wa huduma ya maji wakati huu ambao maeneo mengi huwa ni makavu” Alisema Mhe. Kamwelwe.

Akiunga mkono wazo la Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ambaye alimuomba fedha zinazotumika kuwekea miradi ya maji zitumike kuchimbia visima virefu badala ya kuendelea na miradi hiyo ambayo mbali na kuwa na gharama kubwa huchukua muda mrefu kukamilika na hutoa huduma kwa watu wachache, Mhe. Kamwelewe amesema kuwa kuanzia sasa fedha hiyo ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 500 kwa mwaka zitatumika  kuchimba visima hivyo ili kufikia mwaka 2020 tatizo la maji katika Wilaya hiyo libaki kuwa historia.

“Katika kutekeleza hilo leo ntaacha visima virefu kumi ili tuwe tumeingia kwenye vitendo moja kwa moja huku kila awamu  tutakuwa tukitenga fedha ya kutosha kwa ajili ya kumaliza tatizo la Maji Mkalama” Alisema Kamwelwe.

Akiwa katika kijiji cha Kidarafa kilichopo kata ya Mwanga Mhe. Kamwelwe alivutiwa na maendeleo na mchango unaotolewa na kata hiyo katika uzalishaji wa chakula  na uingizaji wa pato la Wilaya ambapo alisema kuwa mfuko wa maji wa kijiji hicho ni mdogo sana ukilinganisha na gharama ya mafuta ya shilingi laki moja kwa siku jambo ambalo litasababisha jumuiya ya watumia maji wa kijiji hicho kushindwa kumudu gharama za uendeshaji wa mradi huo hivyo alimuagiza  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ampelekee gharama za kuunga umeme wa jua  ili wananchi hao waendelee kupata huduma hiyo ya maji.

“Ninataka baada ya kuweka mitambo ya sola gharama ya maji ishuke kutoka shilingi 50 kwa ndoo mpaka shilingi 20” Aliagiza Mhe. Kamwelwe.

Akimkaribisha  Mhe. Naibu waziri na kuwasilisha  taarifa ya hali ya huduma ya maji kwa Wilaya ya Mkalama Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka amesema kuwa mpaka sasa ni asilimia 43 pekee ya wananchi wa Wilaya hiyo wanaopata huduma  hiyo huku vyanzo vinavyotoa huduma hiyo vikiwa ni 186 kati ya 264 huku vyanzo 78 vikiwa havitoi huduma kutokana na sababu mbalimbali.

“Mhe. Naibu Waziri, Utekelezaji wa miradi mbalimbali Wilayani Mkalama unahusisha wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na Serikali kuu pamoja na  Benki ya Dunia” Aliongeza Mhe. Masaka.

Mhe. Masaka alihitimisha taarifa yake kwa kutaja changamoto mbalimbali zinazoathiri ufanisi wa utoaji wa huduma ya maji Wilayani Mkalama ambazo ni pamoja na Ukosefu wa Vitendea kazi, ufinyu wa bajeti na uchache wa watumishi wa idara ya maji.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe. Allan Kiula alimshukuru Mhe. Waziri kwa kukubali ombi lake na kufika Mkalama ambapo alimhakikishia kuwa ataendelea kushirikina na Wizara yake bega kwa bega ili kuhakikisha malengo ambayo Wizara imeweka juu ya Wilaya ya Mkalama yanatimia.

“Mimi ni Mwakilishi wa wananchi hivyo kila changamoto nayopewa ni lazima niifikishe kwa watendaji na matokeo yake ndio haya na ntajitahidi kuhakikisha  kila Waziri anayehusika na changamoto zilizopo Mkalama anafika hapa ili kujionea mwenyewe hali halisi” Alimalizia Mhe. Kiula.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.