Imeelezwa kuwa ufundishaji mahiri unaozingatia stadi za maisha ni tunu na nguzo muhimu inayomwezesha mwanadamu kujikomboa kifikra kupitia ujuzi ama maarifa kwa lengo la kuendesha maisha yake.
Hayo yameelezwa na mdhibiti ubora wa shule Wilaya ya Mkalama Adam Majid kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wa hojaji wa kujitolea watakaoenda kufanya kazi ya utafiti wa stadi za maisha kwa vijana wa miaka 13 hadi 17.
Bwana Majid amesema kuna ushahidi unaonesha dhahiri kwamba stadi za maisha zimekuwa na matokokeo chanya kitaaluma ikiwemo kuwasaidia vijana kufahamu na kudhibiti hisia zao , kupanga na kufikia malengo chanya , kuhisi na kuonyesha huruma kwa wengine ,kufanya maamuzi sahihi.
Pamoja na hayo aliwataka vijana hao kuwa waaminifu na kufanya kazi kwa weledi na kuwa mabalozi wazuri kuendana na mazingira pamoja na tamaduni za jamii husika Ili kupata utafiti mzuri wa namna vijana hao wanavyoishi na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo pamoja na kutatua matatizo yao binafsi na ya wengine.
Nae Mratibu wa utafiti na upimaji wa stadi za maisha Wilaya ya Mkalama Issa Mtaki amesema zoezi la upimaji wa stadi maisha na Tunu linafanyika kwa umakini mkubwa katika Nchi za Kenya ,Uganda na Tanzania na Kwa Tanzania wilaya 34 ikiwemo wilaya ya Mkalama .
"Zoezi hili limepewa Baraka zote kutoka Kwa viongozi wakubwa na wametupa ushirikiano Mkubwa , zoezi hili linaenda kulenga zaidi kuwapima watoto hasa katika mchakato wa ujifunzaji wa maisha hasa Katika maisha na mazingira yao au shule kwahiyo tukiangalia watoto wenye umri wa miaka 13 hadi 17 ni watoto ambao either wapo shule au nyumbani kwahiyo tunaenda kujua wamepata stadi gani au masuala Gani ya tunu tunayokusudia vijana wetu wapate". Aliongeza Bwana Mtaki.
Pamoja na hayo aliwashukuru mashirika wadau wanaoteleleza mradi huu ambayo aliwataja Milele Zanzibar Foundation , Uwezo Tanzania pamoja na shirika la Mkalama Paralegal ambalo pia linatoa msaada wa kisheria wilayani hapa.
Patrick Immanuel pamoja na Beatrice Mpazi washiriki wa mafunzo hayo wameshukuru kuwa miongoni mwa washiriki ,wamesema watafanya kazi hiyo Kwa uaminifu na wanaamini fursa hii italeta mabadiliko chanya katika maisha hivyo kuwataka jamii kupokea fursa hii Ili watoto waweze kujitegemea wenyewe na kuleta mapinduzi ya kiuchumi ndani ya familia ,Jamii na Taifa Kwa ujumla.
Tangu mwaka 2005 Tanzania ilianzisha mchakato wa kutengeneza Mtaala wa ufundishaji mahiri kwa elimu ya sekondari na mwaka 2007 kwa upande wa elimu ya msingi.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.