Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amezindua mbegu za ruzuku ya Alizeti Kwa Mkoa wa Singida zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bil 8 ambazo zitauzwa kwa wakulima Kwa bei ya ruzuku Ili kuongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo.
Uzinduzi huo umefanyika Januari 3 , 2024 katika ukumbi wa RC Mission Mkoani Singida.
Aidha Mhe. Silinde amesema kuwa Mkoa wa Singida utapokea Tan 600 ya mbegu bora za alizeti, tan 315 za mbegu chotara ambazo sawa na asilimia 42 ya mbegu zote zinazosambazwa Nchini zenye thamani ya Tsh. Bil 6.5 na mbegu za uchavushaji tani 285 zenye thamani ya Tsh.Bil 2.28 nakufanya jumla ya zaidi Tsh bil.8.5 ambazo zitatolewa kwa ruzuku kwa Mkoa wa Singida.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka Wakuu wa Wilaya wote Mkoani hapa kuhakikisha wanafanya usimamizi wa mbegu hizo na kuwafikia wakulima wote ndani ya wiki tatu.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.