Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhe. James Mkwega amewataka madiwani, wakuu wa idara na vitengo kila mmoja kwa nafasi yake kusimamia suala la ukusanyaji wa mapato na kudhibiti mianya ya utoroshaji wa mapato ili kuhakikisha wanatimiza lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Amesema hayo mapema leo katika Baraza la Madiwani la robo ya pili la kujadili utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa kipindi cha Oktoba –Disemba kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
‘’ Ninaomba kila mmoja wetu akitoka hapa akahakikishe anasimamia vyema suala la ukusanyaji wa mapato,wewe diwani kwenye Kata yako hakisha unajua vyanzo vya mapato vilivyopo kwenye kata yako na kudhibiti utoroshwaji wa mazao kwani tayari msimu wa mazao umeanza’’ Alisisitiza Mhe. Mkwega.
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani limeielekeza Halmashauri kupitia Idara ya Kilimo kuwa Maafisa Ugani wawatembelee Wakulima kwa ajili ya kupima afya ya udongo kwa manufaa bora ya kilimo.
‘’ Maisha yetu yanatokana na Kilimo, kwahiyo maafisa ugani mkatumie hizo piki piki mlizopewa kuwahudumia wananchi na sio kuziweka ndani na kila robo tunapokutana hapa nataka taarifa ya maeneo yaliyofikiwa. Aliongeza Mhe. Mkwega.
Sanjari na hayo aliwapongeza watumishi wa Halmashauri na wakuu wa Taasisi Wilayani Mkalama kufanya kazi nzuri kwa robo ya pili ambapo amewasisitiza juhudi walizozifanya kwa robo iliyopita wakafanye vizuri Zaidi katika robo ya tatu.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.