Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Ndugu Abdallah Njelu amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuwaletea vifaa vya kisasa vya TEHAMA kwa ajili ya kufundishia wanafunzi katika kuboresha elimu na ufaulu nchini Tanzania
kauli hiyo ameitoa wakati akimkabidhi Mkuu wa shule ya Msingi Mwalimu Simon Mollel vifaa vya TEHEMA venye thamani ya zaidi ya Tsh 15,000,000 kupitia mradi wa Boost. Makabidhiano hayo yamefanyika leo 13/03/2024 katika ukumbi wa Sheketela wilayani Mkalama
"Kwanza Nimshukuru Mhe Rais Dkt kwa jitihada anazozionesha katika mlengo huu wa TEHAMA. Niwaombe tu vifaa hivi ni gharama kubwa ambayo serikali imeingia, kwahiyo tuvitunze hivi vifaa vituletee tija iliyokusudiwa" Aliongeza Njelu
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nduguti , amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwapatia vifaa hivyo kwani vitasaidia kuboresha elimu na kuongeza ufaulu wilayani Mkalama.
"Tunaishukuru serikali ikiongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu kwa kutuwezesha kupata vifaa hivi vya TEHEMA. Vifaa hivi vitatusaidia kuongeza ubunifu kwa wanafunzi, vitaisidia kutatua changamoto ya uhaba wa walimu na pia vitachangia kuongeza kiwango cha ufaulu ", Mwalimu Mollel.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.