Halmashauri ya wilaya ya Mkalama inatarajia kufunga mfumo wa GoT-HOMIS katika vituo vya afya 3, Zahanati pamoja na hospitali ya wilaya ya Mkalama katika kuboresha utoaji huduma bora kwa wananchi
Akizungumza wakati wa utoaji mafunzo ya mfumo huo, Afisa TEHAMA Halmashauri ya wilaya y Mkalama Nsajigwa Mwangoka amesema mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika utoaji huduma kwa wagonjwa wanaofika kwa ajili ya matibabu katika hospitali au zahanati wilayani hapa.
"Mfumo huu wa GoT-HOMIS unatumika katika kusimamia na kutoa taarofa za shughuli zote za huduma za afya zinatolewa hospitali au kituo cha afya kwa kurekodi kila hatua tangu mgonjwa anaposajiliwa, kutibiwa na kufanya malipo, vipimo hadi dawa" Nsajigwa Mwangoka
"Mbali na hilo, Mfumo huu pia unatumika kusimamia suala zima la upokeaji na utoaji dawa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya" Nsajigwa Mwangoka, Afisa TEHAMA
Kwa mujibu wa Afisa TEHEMA, zoezi hilo la ufungaji mfumo huo limeanza 09/05/2024 katika zahanati ya Igugono na mfumo huo utafungwa katika vituo vyote vya serikali 34 wilayani Mkalama
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.