Vikundi mbalimbali vilivyoomba mkopo unaotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama vyajengewa uwezo wa namna ya kutumia mkopo huo vizuri katika kujiendeleza kiuchumi na kuboresha maisha yao. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bw. Selemani Msunga amevitaka vikundi hivyo kutumia mkopo huo kuboresha maisha yao huku akiwasihi kurejesha kwa wakati kuwezasha vikundi vingine navyo kupata mkopo huo. ‘’niwasihi kurejesha kwa wakati hasa nyie vijana ili muendelee kujenga imani zaidi na vijana wengine wapate’’ Alisistiza Msunga.
Awali akifungua Mafunzo hayo mratibu wa mafunzo Bw. Yesaya Kayange amewataka wanakikundi kuacha alama nzuri katika jamii kwakufanya kazi kwa bidii na kutumia fursa waliyoipata kwa kubuni miradi itakayoishi kwa vizazi vijavyo. Naye Mwl wa ujasiriamali Bw. Gudluck Mlau amevisisitiza vikundi kuwa wabunifu katika kukuza miradi yao baada ya kupatiwa mikopo na kujua mahitaji ya wateja wao huku wakiendana na kasi yaushindani kwakuwa na miradi au bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja. Katika hatua nyingine Afisa Mahusiano Benk ya NMB John Andrea aliwapa elimu ya kutengeneza faida na kuweka akiba na kutunza fedha kwenye akaunti ili kuepuka kula mtaji. Mafunzo hayo yametolewa Feb 18 2025 katika ukumbi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Usharika wa Nduguti kwa vikundi 76 ambavyo vinatajia kupata mikopo ya 10% hivi karibuni
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.