Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Moses Machali amempa muda wa wiki mbili Meneja wa RUWASA wilaya ya Mkalama kuhakikisha anafanya utafiti wa maji katika Kata ya Ibaga kijiji cha Ibaga yanayotajwa kuhatarisha afya za watumiaji
Ametoa maagizo hayo April 16, 2024 wakati akisikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kata hiyo ambapo amesisitiza kufanyika utafiti wa kina kujua chanzo cha kisima hicho kutoa maji yaliyochanganyikana na tope.
‘’ Nakupa wiki mbili Meneja na timu yako tokeni mkafanye uchunguzi kwenye njia zote mlikolaza mabomba ili kubaini tatizo la maji kutoka yakiwa na tope mniletee ripoti ili tuone namna ya kuwasaidia hawa wananchi’’ Alisisitiza Dc Machali.
Mhe. Machali amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani,usalama baina ya mtu huku akiwasisitiza kila mmoja kufanya kazi kwa bidi ili kuunga mkono juhudi za serikali iliyokusudia kuwaletea wananchi katika maeneo yao.
Sanjari na hayo amewataka kulinda miundombinu ya barabara katika kipindi hiki cha mvua kwa kuchukua tahadhari na kuelekeza maji pembeni ili yasiharibu barabara ambayo kwa baadhi ya maeneo yamekata mawasiliano baina ya kitongoji na kitongoji.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.