Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl Doroth Mwaluko amewataka wasimamizi wa Programu ya Shule bora inayotekelezwa katika Mikoa Tisa Nchini kutengeneza mfumo wa kutoa mafunzo kwa walimu wa Mkoa wa Singida ili kuinua kiwango cha elimu Mkoani hapa.
Ameyasema hayo January 31, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida wakati akifungua mkutano wa uhamasishaji wa program ya Shule bora kwa wasimamizi na wahariri wa vyombo vya Habari Mkoani Singida.
‘’Msiwe na kituo cha mafunzo sehemu moja , mnatakiwa kuwa na kituo walau kila Halmashauri kuwe na ‘trainers’ Pamoja na vituo vya kufanyia mafunzo na kuwakutanisha walimu wengi ili wote waguswe kwa wakati mmoja ‘’ Alisema Mwl Mwaluko
Aidha Mwl Mwaluko alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza waandishi wa Habari Mkoani Singida katika kuelekea kilele cha miaka 60 tangu kuanzishwa kwakwe , kuandika Habari na Makala za kutangaza vivutio vilivyopo ndani ya Mkoa Pamoja na zile zitakazosaidia kutatua changamoto kwenye jamii kuliko zinazochochea mifarakano inayorudisha nyuma maendeleo ya Wananchi.
Meneja mawasiliano wa Mradi wa Shule bora Bw. Raymond Kanyambo alisema ili kubaini changamoto zinazo kwamisha ujifunzaji na ufundishaji wa Watoto wa elimu ya Msingi na awali na kuzitafutia utatuzi lazima wasimamizi , wawakilishi na wahariri wa vyombo vya Habari Mkaoni Singida kushiriki kikamilifu katika program hiyo kwakuandika na kuripoti changamoto na vikwazo vinakwamisha Watoto kushindwa kupata elimu bora hapa Nchini.
Kanyambo amesema kwenye program hiyo kundi la waandishi wa Habari litakuwa msaada mkubwa endapo litashirikiana kikamilifu na Shule bora kuzibaini changamoto zinazokwamisha ujifunzaji na ufundishaji wa Watoto shuleni hivyo akatoa wito kwa waandishi wa Habari kuwajibika katika hilo.
‘’ Tunategemea mtashiriki vyema katika program hii kuzibaini changamoto zinazopelekea Watoto wasisome ama wasipate elimu bora na kisha itafutwe njia ya kuondoa changamoto hiyo kama waandishi mnahaki ya kuhoji hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa ngapi wameripoti wangapi wamefaulu, je kundi lenye ulemavu lipo vipi kitaaluma? Hivyo mshirikiane na sisi katika kuinua elimu kwa Watoto wetu’’ Aliongeza Kanyambo.
Aidha alieleza malengo ya programu ya Shule bora kuwa ni Pamoja na kuboresha ujifunzaji kwa Watoto wote shuleni , kuhakikisha Watoto wote wanaenda shule na kusoma , kuboresha ufundishaji wa Walimu ili wawawezeshe Watoto kupata elimu bora , ujumuishwaji wa Watoto wote shuleni kuhakikisha wanapata elimu bora katika mazingira salama na wezeshi, Pamoja na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa elimu ambapo kundi hili linalenga Viongozi wa Halmashauri , Maafisa Elimu Pamoja na Wathibiti ubora.
Mratibu wa Mradi huo Mkoa wa Singida Samweli Danieli alisema kuwa programu hii inalenga elimu ya awali na Msingi na tayari umeanza kutoa mafunzo kwa walimu kazini yajulikanayo kama MEWAKA na hadi sasa Walimu Wakuu , Mahiri na Taaluma 1774 wamenufaika na mafunzo hayo.
Shule bora ni programu ya serikali chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza inayotekelezwa katika Mikoa Tisa Nchini , program hiyo inagharimu Paundi milioni 89 ambazo ni sawa na Billioni 271 za Kitanzania ambazo zitatumika kuinua ubora wa elimu katika mikoa hiyo na kuhakikisha Watoto wote hata wale wenye changamoto wanapata elimu.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.