• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

PROGRAMU YA SHULE BORA ITOE MAFUNZO KWA WALIMU WOTE ILI KULETA TIJA KATIKA SEKTA YA ELIMU

Imewekwa kwenye: February 2nd, 2023



Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl Doroth Mwaluko amewataka wasimamizi wa  Programu ya Shule bora inayotekelezwa katika Mikoa Tisa Nchini  kutengeneza mfumo wa kutoa mafunzo  kwa walimu  wa Mkoa wa Singida  ili kuinua kiwango cha elimu Mkoani hapa.

Ameyasema hayo January 31, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida wakati akifungua mkutano wa uhamasishaji  wa program ya Shule bora  kwa wasimamizi na wahariri wa vyombo vya Habari Mkoani  Singida.

‘’Msiwe na kituo cha mafunzo sehemu moja , mnatakiwa kuwa na kituo walau kila Halmashauri kuwe na ‘trainers’ Pamoja na vituo vya kufanyia  mafunzo na kuwakutanisha walimu  wengi ili wote waguswe kwa wakati mmoja ‘’ Alisema Mwl Mwaluko


Aidha Mwl Mwaluko alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza  waandishi wa Habari Mkoani Singida  katika kuelekea kilele cha miaka 60  tangu kuanzishwa kwakwe , kuandika Habari na Makala za kutangaza vivutio vilivyopo ndani ya Mkoa Pamoja na  zile zitakazosaidia kutatua changamoto  kwenye jamii kuliko zinazochochea mifarakano inayorudisha nyuma maendeleo ya Wananchi.


 Meneja mawasiliano wa Mradi wa Shule bora  Bw. Raymond Kanyambo  alisema ili  kubaini changamoto zinazo kwamisha ujifunzaji na ufundishaji  wa Watoto wa  elimu ya Msingi na awali  na kuzitafutia utatuzi lazima  wasimamizi , wawakilishi na  wahariri wa vyombo vya Habari Mkaoni Singida  kushiriki kikamilifu katika program hiyo  kwakuandika na kuripoti changamoto  na vikwazo  vinakwamisha Watoto kushindwa kupata elimu bora hapa Nchini.


Kanyambo amesema kwenye program hiyo kundi la waandishi wa Habari litakuwa msaada mkubwa endapo litashirikiana kikamilifu na Shule bora kuzibaini changamoto zinazokwamisha ujifunzaji na ufundishaji wa Watoto shuleni hivyo akatoa wito  kwa waandishi wa Habari kuwajibika katika hilo.


‘’ Tunategemea mtashiriki vyema katika program hii kuzibaini changamoto zinazopelekea Watoto wasisome ama wasipate elimu bora na kisha itafutwe njia ya kuondoa changamoto hiyo kama waandishi mnahaki ya kuhoji hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa ngapi wameripoti  wangapi wamefaulu, je kundi lenye ulemavu lipo vipi  kitaaluma? Hivyo mshirikiane na sisi katika kuinua elimu kwa Watoto wetu’’ Aliongeza Kanyambo.


Aidha alieleza malengo ya programu ya Shule bora kuwa ni Pamoja na kuboresha ujifunzaji kwa Watoto wote shuleni , kuhakikisha Watoto wote wanaenda shule na kusoma , kuboresha ufundishaji wa Walimu ili wawawezeshe Watoto kupata elimu bora , ujumuishwaji wa Watoto wote  shuleni kuhakikisha wanapata elimu bora  katika mazingira salama na wezeshi, Pamoja na kuimarisha mifumo  ya usimamizi wa elimu ambapo kundi hili linalenga Viongozi wa Halmashauri , Maafisa Elimu Pamoja na Wathibiti ubora.


Mratibu wa Mradi huo Mkoa wa Singida Samweli Danieli alisema kuwa programu hii inalenga elimu ya awali na Msingi na tayari umeanza kutoa mafunzo kwa walimu kazini yajulikanayo kama MEWAKA  na hadi sasa Walimu Wakuu ,  Mahiri na Taaluma 1774 wamenufaika na mafunzo hayo.


Shule bora ni programu ya serikali chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza inayotekelezwa katika Mikoa Tisa Nchini , program hiyo inagharimu Paundi milioni 89 ambazo ni sawa na Billioni 271 za Kitanzania ambazo zitatumika  kuinua ubora wa elimu katika mikoa hiyo  na kuhakikisha Watoto wote hata wale wenye changamoto wanapata elimu.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.