Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka amekabidhi jumla ya pikipiki 17 zilizotolewana shirika lilisilo la kiserikali linalojulikana kama “EQUIP-T” ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na shirika hilo kama sehemu ya kuwapa hamasa maafisa elimu kata wilayani hapa.
Hafla hiyo fupi ilifanyika mapema leo asubuhi kwenye viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ambapo Mhe. Masaka aliwataka maafisa elimu hao kuhakikisha wanatumia vyombo hivyo vya usafiri kuinua kiwango cha elimu wilayani Mkalama.
“Pikipiki hizi sio za matumizi binafsi na msizitumie kwenda kwenye michepuko yenu kwa sababu tunahitaji kuona pikipiki hizi zinapunguza idadi ya mimba shuleni na zinaongeza kiwango cha ufaulu” Alisisitiza Mhe. Masaka.
Kwa upande wake mwakilishi wa maafisa elimu kata hao ambaye pia ni Afisa elimu kata wa kata ya Msingi, Bw. Elisante Mbazi aliishukuru serikali na shirika la EQUIP-T kwa vitendea kazi hivyo ambapo kwa niaba ya maafisa elimu kata wenzake, aliahidi kutumia pikipiki hizo kuongeza kiwango cha ufaulu na kuboresha elimu kwa ujumla wilayani Mkalama.
“Tulikuwa tunapata changamoto ya kuzifikia baadhi ya shule kwa ajili ya ufuatiliaji lakini sasa kupitia pikipiki hizi za kisasa, changamoto hiyo imeisha” Alimalizia Mbazi.
Pikipiki hizo zilizokabidhiwa leo zilikuwa na viambatanishi vyake vyote vya msingi ikiwemo kofia ngumu na ‘’gloves’’ za kuvaa mikononi wakati wa kuendesha.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.