Katika kuongeza umakini wa usimamizi wa mikopo kwa halmashauri zote Nchini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) imesanifu mfumo wa Kieletroniki ambao utawezesha usimamizi wa mikopo unaotokana na asilimi kumi (10%) na kuongeza udhibiti katika ushughulikiaji wa maombi ya mikopo , usimamizi wa vikundi , marejesho ya mikopo na utoaji wa taaarifa mbalimbli.
Kaimu Mkurungezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Abdalla Njelu alisema hayo wakati akifungua kikao kazi cha mfumo wa kielekitroniki ngazii ya wilaya ya siku mbili yaliyoanza leo Juni 14, hadi juni 16 mwaka huu.
Njelu alisema mfumo huo hautabadili utaratibu uliopo kwa mujibu wa sheria bali unaongeza umakini katika usimamizi wa mikopo kwa kubaini watumishi wasio waadilifu kuchukua mikopo kupitia mgogo wa kikundi, usimamizi usioridhisha wa mikopo inayotolewa , mtu mmoja kukopeshwa zaidi ya mara moja pamoja na marejesho kutorejeshwa kwa wakati na hakuna mkakati wa kusimamia vikundi visivyorejesha kwa wakati.
‘’Ili kuleta ufanisi wa usimamizi wa mikopo hii julai 2018 serikali ilifanya marekebisho ya sheria za fedha za serikali za mitaa sura 250 kwa kuongeza kifungu 37A ambachokimeeleza utaratibu wa utengaji ,utoaji na usimamizi wa mikopo mwaka 2019 OR TAMISEMI iliandaa kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa makundi ya wanawake vijana na watu wenye ulemavu kwa lengo lakufafanua utekelezaji wa sheria hiyo aidha mwezi februari 2021 kanuni hizo zilifanyiwa marekebisho’’ alisema Njelu.
Awali akizungumza kwenye mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mkalama, Mohmed Atiki alisema mfumo huo wa kielekitroniki ujulikanao kama (Ten Percent Loan Management Information System ) utarahisisha utendaji kazi na ufuatiliaji pia kuongeza umakini katika kufuatilia vikundi vyote na kutoa mafunzo kwa maafisa maendeleo ngazi ya kata hadi kwa vikundi na wanatarajia kutoa mafunzo hayo ngazi ya vitongoji.
Pamoja na hayo alisema mfumo huo utabaini vikundi hewa pamoja na mianya yote ya ubadhilifu na kuondoa changamoto zilizokuwa zikijitokeza hapo awali ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wasio waadilifu kutumia vikundi hivyo kwa masilahi yao binafsi.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.